Mashindano yanayoendelea kwa kujumuisha timu 10 kwa michezo ya raundi ya kwanza yameendelea kupamba kasi katika mji wa haydom huku timu inayofungwa inafungasha virago na kupisha mashindano hayo.
timu zote zikipeana mikono ya kutakiana kheri kabla yakuanza mchezo
Katika mchezo wa tatu uliopigwa leo 15/03/2018 katika dimba la shule ya msingi uki zikutanisha timu mbili, huku timu inayoundwa na vijana wajasiliamali wa studio au maarufu kama wapiga picha(Makulusa) leo wameambulia patupu mara baada ya kukubali kipigo cha magori 3-0 kutoka kwa wapinzani wao Airpot FC.
mfungaji wa Goli la kwanza la Airport Fc Abubakari akishangilia kwa nguvu
Mchezo huo ulioanza kwa kasi zaidi ambapo iliwachukua dakika 4 ya mchezo Airtop Fc kupata bao kwa njia ya penati kupitia kwa mchezaji Abubakari Mahina jezi namba 02 mgongoni mara baada ya mlinzi kucheza mchezo usiokuwa wa kiungwana katika eneo la hatari,goli hilo lilidumu kwa takribani dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Kufuatia makosa yaliyoendelea kufanywa na wachezaji wa timu ya Makulusa fc na kuruhusu kushambuliwa kwa dakika 10 za kipindi cha pili mara tu baada ya kuanza mchezo, timu ya Airpot iliendeleza mashambulizi ya kasi huku wakilisakama goli la wapinzani wao na hatimaye kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 60 ya mchezo huo kupitia mchezaji Emanuel Mallo(02) mara baada ya safu ya ulinzi kutoelewana.
baadhi ya mashabiki waliojitokeza uwanjani wakiwa juu ya miti ilikufurahia kandanda safi iliyokuwa inaendelea
Timu zote ziliendelea na mchezo mnamo dakika ya 20 kipindi cha pili, Makulusa walifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji kwa mtoa beki wake wakushoto Regi Naftali na kuingia Yotam Michael, na uku Kulwa Yusuph akitolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Joseph Siasi. Kwa upande wa wapinzani wao walifanya mabadiliko kwa kutoa wachezaji wawili Eliasi Diyomati na Yuda sulle uku nafasi zao zikichukuliwa na Peter Emanuel na Kasimu Rama.Dakika ya 63 ya mchezo Makulasa walipata penati iliyopigwa na Sulle Gimpa na kuokolewa na mlinda mlango.
benchi la ufundi la Makulusa wakitaaruki mara baada ya mchezaji kukosa penati
Mnamo dakika ya 65 ya mchezo yule yule mfungaji wa bao la pili Emanuel Mallo aliwanyanyua washabiki tena kwa kuandika bao safi la kichwa lililomshinda golikipa na kubaki ameduwa kufuatia pasi safi toka kwa Ibrahim Petro. Mchezo uliendelea kwa kushambuliana na timu ya Makulusa walifanya mabadiliko yakumtoa mlinda mlango wao Yoel Peter na kuingia Fakii Massay.
Dakika ya 78 ya mchezo mchezaji wa timu ya makulusa Shija Charles alizawadiwa kadi ya njano baada ya kumchezea Samwel naftali mchezo usio wakiungwana.
Mchezaji wa Makulusa FC akipatiwa matibabu na Madaktari wetu mara baada ya kuhumia
Mara baada ya dakika 90 kumalizika,timu ya Airpot Fc inaungan na timu ya Dongobesh, Stand United kuelekea nusu fainali uku wakisubiri washindi wa mchezo wa kesho tarehe 16/05/2018 kati ya Young boys dhidi Qashash utakaopigwa saa nane mchana na Rema 100 dhidi ya Rambo utakaochezwa saa 10 jioni.
mashabiki waliokuwa wamekaa jukwaa kuu wakiendelea kufuatilia mchezo
Mashindano ya Kurugenzi Cup’18 yanendelea katika mji wa haydom ikiwa wiki ya kudhimisha tamasha la Ujasiliamali, Uwajibikaji na Uzalendo litakalo hitimishwa tarehe 20/05/2018 kwa kupewa mada mbalimbali za ujasiliamali toka kwa wabobezi wa masomo hayo.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.