BARAZA la Mitihani Tanzania (Necta) leo limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.29 kutoka asilimia 77.09 mwaka 2017 hadi asilimia 78.38.
Wanafunzi 57 wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Tumaini Lutheran Seminari ya Malinyi mkoani Morogoro wamefutiwa matokeo baada ya kubaini shule hiyo ilivujisha mtihani huo.
Mbali na kufuta matokeo hayo, Necta imekifungia kituo hicho cha kufanyia mtihani.
Hayo yameelezwa leo Alhamisi Januari 24, 2019 na Katibu Mkuu mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 mkoani Dodoma.
Msonde ameagiza wahusika wote kuchukuliwa hatua wakiwemo polisi waliosimamia.
SHULE KUMI BORA KITAIFA
1. ST. FRANCIS GIRLS
2. KEMEBOS
3.MARIAN BOYS
4.AHMES
5.CANOSSA
6. MAUA SEMINARY
7. PRECIOUS BLOOD
8. MARIAN GIRLS
9. BRIGHT FUTURE GIRLS
10. BETHEL SABS GIRLS
SHULE KUMI ZA MWISHO KITAIFA
1. Pwani Mchangani -Kaskazini Unguja
2. Ukutini – Kusini Pemba
3. Kwediboma – Tanga
4.Rwemondo – Kagera
5. Namtula – Lindi
6.Kijini -Kaskazini Unguja
7.Komkalakala -Tanga
8.Kwizu – Kilimanjaro
9. Seuta -Tanga
10. Masjid Quban Muslim – Dar es Salaam
KUTAZAMA MATOKEO HAYO YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU BOFYA HAPA:- https://www.necta.go.tz/results/2018/psle/results/distr_2104.htm
KUTAZAMA MATOKEO HAYO YA HALMSHAURI YA MJI WA MBULU BOFYA HAPA:- https://www.necta.go.tz/results/2018/psle/results/distr_2107.htm
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.