Ikiwa ni bonanza la michezo lililowakutanisha watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu dhidi ya Watumishi wa Manispaa ya Singida mnamo tarehe 25/06/2022 kuanzia saa tatu asbh katika Viwanja vya shule ya Msingi Mwenge Singida Manispaa.
Timu ya Mpira wa Miguu toka Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
Iliwachukuwa ni dk.32 ya mchezo Mbulu DC kupitia kwa mshambuliaji wao machachali James Mbinga(muuguzi kituo cha afya dongobesh) Kupachika bao la kwanza baada ya kupokea krosi safi toka kwa ndugu John(mwalimu) winga wa kushoto kupeleka mashambulizi katika lango la wapinzani,
Katika bonanza hilo michezo mbalimbali iliweza kufanyika ikiwa ni pamoja na kuvuta Kamba,kuogelea na mpira wa miguu, miongoni mwa michezo ulioweza kuvuta na kupamba bonanza ilikuwa ni Mpira wa Miguu kwani ulikuwa na upinzani sana toka pande zote mbili licha ya Singida manispaa kuambulia kichapo cha mabao matatu(3) kwa yai(0) toka kwa wapinzani wao ambao ni watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Baadhi ya Wachezaji wa Timu yakuogelea wakiendelea kufanya mazoezi mepesi kabla ya mashindano
Mnamo dk.62 ya mchezo kipindi cha pili cha mchezo ni yule yule kijana mwenye uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu bwana James Mbinga aliwainua tena mashabiki wa Mbulu DC baada ya kupigwa faulu moja iliyochongwa na mlinzi wa kulia anaye panda na kushuka kama Zimbwe ndugu Florence Hayuma (IT) na kutua kichwani kwa James kisha kumuacha mlinda mlango wa Singida manispaa akiokota nyavu.
Daktari wa timu Chris kope toka Mbulu DC akiendelea kufulai jambo baada ya kuona wachezaji wake hakuna majeruhi
Mchezo huo uliendelea kwa kasi sana katika lango la Wapinzani licha ya timu zote mbili kufanya nabadiliko ya hapa na pale, lakini ilikuwa ni dk. 82,ya straika wa mbulu DC bwana Abduli kufanyiwa faulu katika eneo la penati na mwamuzi kuamuru kupigwa penati, alikuwa ni mfamasia toka dongobesh ndugu Menjo Diyamet aliyepiga kwa usatadi na hatimaye kuitimisha kalamu ya magoli.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imekuwa na utamaduni wa kufanya mabonanza mbalimbali ya michezo katika halmashauri mbalimbali hii ikiwa ni sehemu ya kuimarisha afya za wachezaji na kubadilisha mawazo mbalimbali katika utendaji wa kazi.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.