Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James mapema leo ameungana na Mkuu wa wilaya ya Kiteto, kupokea fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 4,740,700,000.00 ikiwa ni faida ya biashara ya hewa ya ukaa inayofanyika kwa uhifadhi wa misitu na mazingira chini ya Usimamizi wa Taasisi ya Carbon Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Dkt. Suleiman Jafo
Akizungumza katika hafla hiyo maalumu ya kukabidhi hundi, Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Dkt. Suleiman Jafo ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Manyara na Wilaya ya Mbulu na Kiteto kwa kusimamia kikamilifu mpango huo ambao umesaidia kubadilisha maisha ya jamii, umechochea utunzaji wa mazingira na umeharakisha huduma kwa Wananchi katika Vijiji vinavyo endesha mpango huo.
Biashara ya Hewa ya ukaa inafanyika wilayani Mbulu katika Halimashauri ya wilaya ya Mbulu, Ikihusisha jamii ya Wahadzabe katikaKata ya Yaeda chini, Maeneo ya Mongo wa Mono, Domanga, Yaeda chini na Heshkesh.
Kupitia biashara hii Wananchi wameweza kutunza na kulinda hifadhi kwa hiyari, Wameweza kujipangia maendeleo yao na kujenga miradi ya huduma, pamoja na kuimarisha Uchumi wao.
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James ameipongeza Carbon Tanzania kwa kazi kubwa wanayo endelea kuifanya kwa kushirikiana na Wananchi, na amewaahidi ushirikiano zaidi ili kuongeza tija na ustawi wa watu na mradi kwa ujumla.
Hafla hiyo maalumu Imehudhuriwa pia na Mheshimiwa Queen Sendiga Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Waheshimiwa Madiwani, Wenyeviti wa vijiji na Wananchi wanao ishi katika vijiji vinavyo nufaika na mradi.
#Kwapamoja, Tunaijenga Mbulu yetu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.