Na Ruth Kyelula, Mbulu Dc.
Mbunge wa Mbulu vijijini Flatei Massay, amewataka wananchi wa Garkawe walitumie vizuri josho na kulilinda ili huduma hiyo iendelee kuwasaidia wakazi wote wa Garkawe na vijiji jirani.
Mheshimiwa Flatei aliyasema hayo wakati akifungua josho la Garkawe, lililopo kata ya Maretadu wilayani Mbulu, mnamo tarehe 5 January, 2024.
Mh. Flatei Massay akizungumza na wananchi wa Garkawe mara baada ya uzinduzi wa josho.
“Niwaombe sana wananchi, hii ni ya kwenu muilinde, muichunge na muihifadhi, iende kwa muda mwingi zaidi. Mheshimiwa Rais namshukuru kwasababu ametupa fedha milioni 23 ya kuweza kujenga hili josho. Niwashukuru na ninyi viongozi kwa kweli mlikuwepo hapa na kusimamia shughuli hii ya ujenzi mpaka ikaisha, na pia niwaombe wananchi leo kuna dawa tumenunua ya kuwaanzishia halafu baada ya hapa mtaendelea na utaratibu wenu mtakaojipangia kila mnapotaka kuogesha mifugo.” Alisema Mhe. Flatei.
Naye Afisa Mifugo Nicodemus Michael alisema kuwa anamshukuru Mheshimiwa Rais na Mbunge wa Mbulu vijijini kwa msaada huu wa mradi wa josho na dawa. Pia aliwaambia wananchi wa Garkawe kuwa utaratibu wa kuogesha mifugo ni kwamba serikali imetoa dawa kama kianzio na baada ya hapo wananchi wenyewe mtatakiwa kununua dawa.
Afisa mifugo, Nicodemus Michael akitoa maelekezo ya namna ya kuogesha mifugo kwenye josho hilo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa kijiji cha Garkawe, Petro Panga alisema kuwa josho lilianza January 2023, alisema wananchi walichanga mchanga, kokoto na mawe kwenye ujenzi huo. Ameishukuru serikali kwa kuwapa milioni 23 kwa ujenzi wa josho hilo la Garkawe.Amesema kwa sasa wanajipanga kuunda kamati ya kusimamia josho hilo.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.