Kutoka Kushoto ni Mh. Mbunge Jimbo la Mbulu Vijijini Flatei Massay, Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini J. Mandoo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar Kuuli Wakiwa Katika Uzindua Huo wa Sensa ya Majaribio ya Watu na Makazi Kata ya Eshkesh Kijiji cha Domanga.
Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini J. Mandoo Akizungumza na Wananchi.
Kutoka Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Bi. S.Sanga.
Mh. Mbunge Jimbo la Mbulu Vijijini Flatei Massay Akimsikiliza Mama wa Kihadzabe Akiongea Katika Mkutano Huo
Hapo Chini ni Watumbuizaji kwa Ngoma za Kiasili Wakifanya Mambo Yao Kma Inavyoonekana Kwenye Picha Katika Mkutano Huo
Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri ya Mbulu Mji na Vijijini Wakiteta Jambo
~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mgeni rasmi huyo Mh. Anna Makinda Spika wa Bunge Mstaafu na Kamisaa wa Sensa Kitaifa, amezindua zoezi hili katika halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Kata ya Eshkesh Kijiji cha Domanga. kimsingi Kijiji cha Domanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini ni miongoni mwa vijiji 13 vya Tanzania nzima na Wilaya 11 nchi nzima ikiwa ni kijiji cha majaribio ya sensa ambayo yanatarajia kufanyika rasmi mwezi Agosti 2022 alisema Kamisaa Mh. Anna Makinda.
Serikali kupitia taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) imeamua kuchukua kijiji hiki kwasababu maalumu ili kuzitambua mapema changamoto za makundi mbalimbali ya vijiji tofauti tofauti kwa nchi nzima ili kwamba changamoto zitakazoonekana kwa sasa hivi basi zitapelekea utatuzi wa mapema ili kuhakaikisha upatikanaji wa takwimu sahihi na kwa wakati kwa watu wote kwa maslahi mapana ya nchi yetu zinawezekana. Sensa hii ni muhimu kwa Taifa kwa kuwa husaidia kufahamu mahitaji ya taifa kwa kila sekta.
Kabla ya kufanya sensa ya watu na makazi, ni kawaida kufanya sensa ya majaribio mwaka mmoja kabwa ili kupima utayari wa serikali katika kufanikisha kazi hiyo zikiwemo nyenzo zitakazotumika yakiwemo madodoso, miongozo na matumizi ya teknolojia ya vishikwambi.
Sensa hii ya majaribio ni maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022. Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathmini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalumu.Hata hivyo, katika kijiji cha Domanga wanapatikana wenyeji wa kabila la wahadzabe na wadatoga ambao maisha yao kwa ujumla ni ya kiasili zaidi kama vile kuishi kwa chakula cha kitamaduni ambacho ni matunda pori, asali, nyama pori na mizizi, hivyo hupelekea shuguli kuu za kijamii na kiuchumi ni uwindaji wa porini. Serikali katika utekelezaji wa jaribio hili kwa jamii hii ya wahadzabe na wadatoga watatafuta kitoweo kitakachowafaa kama kihamasisho ili waweze kufanikisha upatikanaji wao na ushrikiano wa kutosha.
Zoezi hili linatarajia kuanza tarehe 11.09.2021 kwa Wilaya zote.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.