Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere Akizungumza Katika Mkutano wa Hadhara na Wananchi wa Kitongoji cha Domanga Kijiji cha Eshkesh Kata ya Eshkesh.
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere Akisindikizwa na Mwenyeji Wake Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Katika Kitongoji cha Domanga - Mbulu
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere Akiwasalimia Wajumbe wa Kamati ya Sensa Ngazi ya Kata na Kijiji
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar Abdallah Kuuli na Kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Mbulu Ndugu Sara Sanga
Katibu Tawala Wilaya ya Mbulu Ndugu Sara Sanga Akitambulisha Wajumbe Mbalimbali Katika Kikao Kazi Hicho
Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Akisalimia Katika Kikao Kazi Hicho
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere Akizungumza na Kamati zote za Sensa ya Mkoa, Wilaya, Kata na Kijiji Katika Kikao cha Ndani Kitongoji cha Domanga
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere Akisindikizwa na Mwenyeji Wake Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Wakiwasili Katika Uwanja wa Mkutano wa Hadhara Katika Kitongoji cha Domanga - Mbulu
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere Akiwa na Wananchi wa Domanga Akicheza Ngoma za Kienyeji
Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu J. Mandoo Akisalimia Katika Mkutano wa Hadhara
Mh. Diwani wa Kata ya Eshkesh Akisalimia Katika Mkutano wa Hadhara
Mh. Mbunge wa Jimbo la Mbulu Flatei Massay Akisalimia Katika Mkutano wa Hadhara
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Akimkaribisha Mh. Mkuu wa Mkoa M. Nyerere
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere Akimkabidhi Zawadi ya TSh. 100,000.00 Mwakilishi wa Kina Mama wa Kihadzabe na Kigatoga.
~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~
Haya yamejiri baada ya Mh. Mkuu wa Mkoa M.Nyerere kukutana na wananchi husika kisha kukagua na kujiridhisha maendeleo ya zoezi hili katika Kata ya Eshkesh Kijiji Eshkesh Kitongoji cha Domanga zoezi lililoanza tarehe 11.09.2021 na litakamilika tarehe 19.09.2021 ambapo kaya zipatazo 110 zinatarajiwa kufikiwa katika udodosaji huu ambapo hadi tarehe 16.09.2021 kaya zipatazo 96 zilikuwa tayari zimeshafikiwa ambayo ni sawa na 87.2% ambayo kitaifa Mkoa wa Manyara Wilaya ya Mbulu inaongoza hadi sasa.
Msafara wa Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere uliopokelewa na mwenyeji wake Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Sezaria V. Makota ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa na Makazi ngazi ya Wilaya ulipokelewa kwa nderemo, hoihoi na vifijo vilivyoshajiishwa zaidi na nyimbo za kienyeji za kihadzabe na kigatoga kitu ambacho ilikuwa ni furaha sana kwa wenyeji hawa kutembelewa na Mh. Mkuu wa Mkoa Huyu.
Mafanikio haya yametokana na usimamizi mzuri wenye mikakati suluhishi ya changamoto za sensa kwaeneo husika ambapo ushirikishwaji wa wazee maarufu ambao ni wenyeji kuwasikiliza wanahitaji kitu gani ili kufanikisha zoezi hili ambao nao walisema watahitaji nyama pori aina ya nyumbu, kitoweo ambacho kilipatikana kwa wingi baada ya serikali kuwa sikivu na kuridhia kuwafanyia hivyo wananchi wake kwa maslahi mapata ya Taifa. Katika Mkutano mkuu wa hadhara uliojaa pomoni kwa wananchi hawa Mh. Mkuu wa Mkoa M. Nyerere amewaomba wenyeji hawa waendelee kutoa ushirikiano wa dhati kazi zoezi hili.
Katika kuhitimisha Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Sezaria V. Makota amemshukuru Mh. Mkuu wa Mkoa M. Nyerere kwa kushiriki katika mkutano huu na anaishuruku serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mh.Rais, Samia S.H. kwa kuendelea kuwajali wananchi wa Wilaya ya Mbulu kwa kuleta fedha za miradi mbalimbali kama vile ujenzi wa kituo cha Afya Kata hii ya Eshkesh kilichopokea kiasi cha Tsh. Milioni 400 ambapo ujenzi unaendelea, ujenzi wa daraja nao unaendelea kata hii hii. Lakini changamoto kubwa ni ya maji ambapo Mh. Mkuu wa Mkoa amelipokea na ametamka atalifanyia kazi na kipindi atakaporudi kutembelea miradi Wilaya ya Mbulu basi atakuwa na majibu ya kero hii.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.