Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere Akizungumza Katika Baraza Maalumu la Madiwani Lililojadili Hoja za Ukaguzi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Katika Kikao Kilichofanyika Ukumbi wa Gote, Dongobesh - Mbulu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga Akitambulisha Makundi Mbalimbali Katika Kikao Hicho.
Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Chelestino Simbalimile Mofuga Akitoa Salamu Katika Kikao Hicho.
Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mh.J.G.Mandoo Akifungua Kikao cha Baraza Hilo.
Mlezi wa Mkoa wa Manyara kwa Serikali za Mitaa Toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Kibasa Akizungumaza Katika Kikao Hicho.
Mwandishi wa Vikao Vya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Mlokozi Akisoma Hoja Mbalimbali za Ukaguzi Katika Kikao Hicho.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bw. Kaganda Akizungumza Katika Kikao Hicho.
Picha za Wah. Madiwani
Picha za Wataalam
Picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga na Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere Baada ya Kikao Hicho
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Haya yamejiri leo tarehe 03.06.2021 katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kilichohusu kujadili hoja zilizoibuliwa na Mkaguzi Mkuu wa serikali za mitaa kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika katika kituo cha elimu cha Gote kilichopo Kata ya Dongobesh Wilayani Mbulu.
Mh. Mkuu wa Mkoa M.Nyerere amesema ni heshima kubwa sana kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa nikiwa mtoto wa Rais wa baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere na kwamba watu wote wasiwe na wasiwasi mimi ni mwakilishi wa Mh.Rais Samia Suluhu Hassan hivyo niko kwa ajili yenu naomba mnitume.
Aliongeza kwa kusema lazima kuongoza vizuri, tusiwaongoze vibaya kwani kila ngazi ya uongozi itawaharibia walioko chini yao kwani hiyo kwa wale wa ngazi ya mwisho ujue kabisa watawanyayasa wananchi.
Mh. Rais alikaa na wazee wa Dar es salaam kwa niaba ya wazee wote nchini, akiwaambia mambo kadhaa ya msingi likiwemo kuwabadilisha baadhi ya viongozi katika ngazi mbalimbali kwa nia njema kabisa ya kuboresha utendaji kazi wa kila siku wa serikali hivyo msiwe na hofu kila kitu kinakwenda vizuri.
Kwa mujibu wa sheria namba 19 kifungu cha 5 Mkuu wa Mkoa atasimamia shuguli zote za ndani ya Mkoa husika kwa maendeleo mapana ya watu wake ikiwa ni pamoja na kufuatilia matumizi na mapato ya wilaya zote katika Mkoa ninaousimamia.
Katika taarifa ya Mkaguzi ya hesabu kama ilivyowasilishwa na Mkaguzi wa hesabu za serikali za mitaa kwa mkoa wa manyara ni kutoa maoni huru kwa hesabu za Halmashauri ili kujiridhisha kama fedha zilizokusanywa zilitumika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu sahihi. Pia kwa upande wa manunuzi ni kujiridhisha kama manunuzi husika yalifuata sheria, kanuni na taratibu za manunuzi.
Katika miradi ya maendeleo ukaguzi unafanyika kuangalia ubora wa miradi husika kama inaendana na thamani halisi ya fedha iliyotumika. Kitu ambacho ni sahihi kabisa kwa hiyo siyo kukosoa tu bali ni kushauri nini cha kuboresha ili kuimarisha mifumo ya makusanyo ya fedha, matumizi, na usimamizi wa miradi hii katika uwekezaji ili wananchi wapunguziwe kero mbalimbali zinazowakabili. Mh. Mkuu wa Mkoa M.Nyerere ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa kupata hati safi kwa miaka 3 mfululizo haya ni matokeo mazuri ya utendaji kazi kati ya madiwani na wataalam wa halmashauri ya wilaya ya Mbullu.
Hata hivyo maeneo yenye mapungufu yafanyiwe kazi na hoja hizi 11 zilizobaki za mwaka wa fedha 2019/2020 ziendelee kufanyiwa kazi ili ziishe. Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ameahidi anapanga kutembelea kila Wilaya katika Mkoa huu siku 5 kwa kila Wilaya kukagua na kujadiliana kero, changamoto na namna ya kuzitatua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga ameishukuru sana Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendekea kuwajali wananchi wa Halmashauri ya Mbulu kwa kuleta fedha nyingi ambazo hazikuwepo kwenye bajeti kwa baadhi ni milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Kata ya Eshkesh, milioni 220 kwa ajili ya zahanati kisha milioni 210 kwa ajili ya ununuzi wa gari la mkurugenzi.
Viongozi wote Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. HUdson Kamoga, Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mh. Flatei, Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mh.J.G.Mandoo na Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Chelestino Simbalimile Mofuga wamemueleza Mh. Mkuu wa Mkoa changamoto zilizopo kubwa ni uchache wa watumishi katika idara mbalimbali lakini idara zilizoathilika sana ni Ujenzi kwa kutokuwa na Mkadiriaji wa Majengo "Quantity Surveyor" lakini pia Mhandisi wa Ujenzi kuwepo 1 anachoka sana hivyo kupelekea baadhi ya miradi kuchelewa kuanza kwa sababu hana muda wa kufika eneo husika kutokana na miradi kuwa mingi sana. Idara ya Pili ni ya Fedha na biashara wapo wahasibu wawili tu mpaka sasa hivyo ukusanyaji wa mapato kuwa shida na viti vingine vya kitaalamu kufanywa kwa kutumiamuda mrefu sana kutokana na uchache huu wa watumishi.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.