Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Akifungua Kikao Kazi cha Kamati ya Sensa na Makazi ya Majaribio Ngazi ya Wilaya Katika Ukumbi wa Kituo cha Elimu cha Gote, Mbulu - Dongobesh
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Akifungua Kikao Kazi cha Kamati ya Sensa na Makazi ya Majaribio Ngazi ya Wilaya Katika Ukumbi wa Kituo cha Elimu cha Gote, Mbulu - Dongobesh
Aliyesimama ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar Abdallah Kuuli Akizungumza Katika Kikao Hicho.
Aliyesimama ni Mratibu wa Sensa Wilaya ya Mbulu Bw. Bashage Bura Akiwasilisha na Kutoa Ufafanuzi Taarifa ya Zoezi la Sensa na Makazi la Majaribio Katika Kikao Hicho.
Wajumbe wa Kamati ya Sensa na Makazi ya Mjaribio Ngazi ya Wilaya Wakiwa Katika Kikao Hicho.
~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Sezaria V. Makota ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa na Makazi ngazi ya Wilaya amepokea taarifa hiyo mbele ya kamati husika iliyokuwa na kikao kazi katika ukumbi wa kituo cha elimu cha Gote Kata ya Dongobesh Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu. Amesifu uwasilishaji huu wa mratibu wa sensa Wilaya Bw. Bashage Bura, utendaji kazi wa timu nzima ya wataalamu na makarani wao katika zoezi hili la sensa.
Katika mawasilisho hayo mratibu huyo Bw. Bashage Bura amesema zoezi hili linaendelea vizuri sana baada ya kuanza tarehe 11.09.2021 ambapo litamalizika terehe 19.09.2021 ambapo hadi kufikia tarehe 16.09.2021 tayari kaya 96 kati ya 110 sawa na 87.2% zilikua tayari zimeshafikiwa.
Mratibu huyu aliendelea kwa kusema Serikali kupitia taasisi ya Takwimu ya Taifa imeamua kuchukua kijiji hiki cha Domanga Kata ya Eshkesh kwasababu maalumu ili kuzitambua changamoto zilizopo kisha kuzifanyia kazi mapema kama vile jografia ya eneo la Kitongoji hiki, mila na desturi za wakazi wa kitongoji cha Domanga yaani wahadzabe na wadatoga na pia shuguli za kiuchumi na kijamii wanazozifanya watu hawa.
"sensa hii ya majaribio ni maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya Agosti, 2022. sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathmini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumimi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalumu. Sensa hii ni muhimu kwa taifa kwa kuwa husaidia kufahamu mahitaji ya Taifa kwa kila sekta katika nyanja mbalimbali.
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Sezaria V. Makota ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa na Makati ngazi ya Wilaya amesisitiza kwa wataalamu na kamati kwa ujumla wao kuendelea kuwa na ushirikiano, kusaidiana kwa dhati ili kufikia 100% ya kaya zinazohitajika kufikiwa hapo tutakuwa tumefikia malengo yaliyokusudiwa.
Hata hivyo, baada ya kujua hali halisi ya maeneo yetu pamoja na Kitongoji cha Domanga tutaweza kufanya maamuzi sahihi ya nini serikali ifanye ili kusaidia wananchi kulingana na matokeo ya sensa hii na ya mwakani.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.