~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Haya yamejiri leo katika kikao cha Kamati ya UVIKO 19 ya Wilaya ya Mbulu Vijijini kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ambaye Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Alikuwa ndiyo mwenyekiti wa Kikao na kamati hiyo.
Katika Kikao hicho wakufunzi ni wataalamau wa afya toka OR - TAMISEMIM, mkoani Manyara na Halmashauri ambao wamebobea katika masuala ya utabibu na mafunzo ya chanjo pia. Wahusika katika kikao hiki ni Wataalamu wa afya, baadhi ya wakuu wa Idara na vitengo, wazee maarufu, mwakilishi wa wafanya biashara, viongozi wa dini mbalimbali, kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya.
Hii imepelekea wahusika walioshiriki kikao hicho kupata elimu ya UVIKO 19 kwa kina na pina.kimsingi hadi kufikia jaana tarehe 26.09.2021 Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini imechanja watu wapata 514 huku zoezi la uhamasishaji kimkakati linaendelea kwa kasi kuanzia kwenye mikutano ya vijiji na vitongoji ya hadhara, minada na baadaye nyumba kwa nyumba, huku vituo vyote 26 vya kutolea huduma ya afya vinatoa pia chanjo ya UVIKO 19 bure kabisa.
Katika kuhakikisha watu wote wanaelewa kwa undani ni kwamba chanjo hii ni salama, na serikali inawajali wananchi wake ndiyo maana inafanya hii chanjo kuwa ya muhimu kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Chanjo hii ilitathminiwa na chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) kwa kutumia wataalamu waliotopea na kubobea katika chanjo huku wakitumia vifaa vya kimamboleo vyenye teknolijia ya kisasa vya kuchanganua kwa undani chanzo husika.
Aina ya chanjo zilizoidhinishwa baada ya uchambuzi huu ni Pfizer-BioNTech, Moderna, Oxford-AstraZeneca, Sinopharm na Johnson & Johnson ambapo kwa sasa chanjo iliyopo ni Johnson & Johnson ndiyo inayochanjwa kwa sasa hapa Tanzania na hizo zingine zitafika kwa hapo baadaye.
Kuna mambo 3 ya msingi nayo ni kwanza utafiti ulianza tangu miaka ya mwanzoni mwa 2000 ambapo kulitokea na ugonjwa wa virusi kama huo yaani SARS, MERS na mengine mengi kiasi kwamba aina ya kirusi huyu wataalam walifanya utafiti wa kutosha kwa wakati huo ila waliacha kuendelea na utafiti baada ya ugonjwwa husika kupotea katika nzchi za urabuni. Lapili ni kutumika kwa vifaa na teknolojia ya kisasa ambapo kwa zamani ingechukua muda mrefu sana kuchambua nini hasa mdudu tabia za mdudu husika na tumthibiti vipi. Cha tatu ni ugonjwa kuenea kwa kasi kwa binadamu hivyo kupelekea hata utafiti wa ugojwa huu kwenda haraka kwasababu ya kupata majibu kwa watu wengi zaidi wanaougua kwa muda mfupi, Cha nne ni kuona watu wanafariki sana hivyo kupelekea kuwepo kwa hii chanzo ili kunususru maisha ya wananchi duniani.
chanjo hii ni salama kwa rika na jinsi tofauti kama vile wazee, kina mama, vijana, wenye magojwa sugu na haina madhara hata kwa mwanamke mwenye mimba na anayenyonyesha ndiyo hasa inamkinga na mtoto pia.
watu wanapaswa kuchanjwa kwasababu ya kuongeza kinga, na kutokuwa mbebaji wa virusi kupeleka kwenye familia, wagonjwa wengine hospitalini, wanafunzi, abiria wanaosafiri kwenye vyombo mbalimbali, kulinda watalii na hatimaye kuuwezesha uchumi wa nchi yetu kutoporomoka zaidi, kwani hakuna mtalii kutoka nje atapenda atumie usafiri ambao anajua wahusika hawajachanjwa.
Hata hivyo Mh. Mkuu wa Wilaya huyo, ameishukuru serikali kwa kuwajali wananchi wa Wilaya ya Mbulu hadi kuwaletea chanjo hii kwa maslahi mapana ya familia zao na taifa kwa ujumla, hivyo kama Wilaya tuko kimkakati zaidi tunahamasisha kwa kila mtu kuchanjwa ili tuvuke lengo la 60%. Na amewaasa wataalamu wa afya na kamati ya UVIKO 19 kwa ujumla wao kwamba ni lazima uchanjwe wewe muhusika ili uwe balozi mzuri wa kuwahamasisha wananchi kupata chanjo.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.