Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria Veneranda Makota Akifungua Mafunzo Hayo Katika Ukumbi wa Kituo cha Elimu Gote, Dongobesh - Mbulu.
Kutoka Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Michael Faray, Anayefuata ni Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Joseph Guulo Mandoo na Aliyesimama ni Mgeni Rasmi Ambaye ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria Veneranda Makota Akifungua Mafunzo Hayo na wa Mwisho ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Bi. S.Sanga.
Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Joseph Guro Mandoo.
Aliyesimama ni Mh. Mbunge, Flatei Jimbo la Mbulu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Michael Faray.
Mratibu wa TASAF kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Mosses Nguvava.
Mkufunzi Ngazi ya Kitaifa Bw. Mkwizu Akitoa Mada.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mbulu.
Mkamu Mwenyekiti Akiongoza Mjadala Huo Kwenye Mafunzo Hayo.
P
Picha Mbalimbali za Pamoja na Mgeni Rasmi Mh. Mkuu wa Wilaya S.V.Makota.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Katika ufunguzi huo Mh. Mkuu wa Wilaya Sezaria Veneranda Makota amesema, Serikali imepanga Kikao kazi hiki kwa umuhimu wake ili wote tuwe na uelewa wa pamoja yaani madiwani, viongozi na watendaji juu ya utekelezaji wa suala zima la TASAF awamu ya pili kuhusiana na utambuzi wa walengwa wa kaya maskini. Tukiwa na umakini wa pamoja na kupata uelewa mkubwa basi uongozi wetu na utumishi wetu kwa ujumla utakuwa wa kutukuka na hatimaye wananchi wetu wa Wilaya ya Mbulu wataboresha maisha yao.
TASAF ni chombo cha serikali kinachosaidia jitihada za wananchi kuondoa kero za umaskini katika maeneo yao, kazi ambayo sisi sote kwa pamoja tunatakiwa kuifanya. Ni matumaini yangu kuwa kikao kazi hiki kitakua chachu na tija ya kuamsha ari na morali mpya; niwatoe hofu juu ya utambuzi huu kwani tunatarajia watumishi hawa kutenda haki katika zoezi hili kwa manufaa mapana ya Wilaya ya Mbulu na Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo, Mh. Mkuu wa Wilaya Sezaria Veneranda Makota amemshukuru sana Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha kwa ajili ya wananchi wa hali ya chini ili wanufaike na kuwa na maisha ya kujiweza.
Katika risala ya Mkurugenzi wa TASAF Tanzania iliyosomwa na mwakilishi wake, kwanza anamshukuru Mkurugenzi Mtendaji (W) wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Bw. A.Kuuli kwa kutoa wataalamu katika kufanya kazi hii. Kwa taarifa zilizopo ni kwamba tangu kuanzishwa mpango huu TASAF imepunguza kiwango cha umaskini kwa asilimia 10% miongoni mwa jamii za watanzania. Kwa sasa utambuzi huu ni wa muhimu kwani kuna kaya hazikufikiwa kwa awamu za zilizopita hivyo watapatikana kwa awamu hii.
Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha tunashirikiana na wadau wetu ili kumuwezesha mwananchi kuingia katika hatua nyingine ya maendeleo, ni muhimu kuchanganua kwa kina nani ni muhusika mahususi wa kuitwa kaya maskini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, amewaagiza wataalamu wote kutumia weledi wa kutosha ili kuhakikisha kazi haikwami kuanzia mwanzo hadi mwisho. Mh. Mbunge, Flatei wa jimbo la Mbulu Vijijini aliongeza kwa kusema kuna vijiji vingi ambavyo havikuwepo katika mpango wa TASAF ulioisha hivyo anamatumainik kwamba awamu hii watafikiwa.
Katika mafunzo hayo imefahamika kwamba vijiji 28 ndivyo vitakavyofanyiwa kazi ambapo hadi kumalizika zoezi hili la utambuzi basi vitakuwa vimefikiwa jumla ya vijiji 76 katika mpango huu ambapo utadumu kwa muda wa miaka 3 hadi 2023 kwa Tanzania nzima.
Madhumuni ya mpango huu kwa kipindi hiki ni kuwezesha kaya za walengwa kuwaendeleza watoto wao, kuwezesha kaya kuongeza rasilimali zalishi na vitega uchumi endelevu ili kuwa na matokeo chanya ya uzalishaji.
Ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa uwazi na ufanisi zaidi TASAF ina muundo maalumu wa kitaasisi ambapo ni kuanzia Ngazi ya Taifa, ngazi ya mkoa, ngazi ya halmashauri, ngazi ya kata na mwisho ni ngazi ya kijiji hii ni kwa upande wa Tanzania Bara.
Katika kipindi chote cha miaka 3 mpango huu unatarajia kutumia kiasi cha Dola za Marekani (USD) 883.3 ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania 2.03 trilioni zinazochangiwa na Benki ya Dunia na wadau wengine wa maendeleo, ambapo katika utekelezaji huu wa sasa walengwa wote watapokea fedha kwa njia ya kielektroniki kupitia mawakala wa kibenki, ambapo hadi sasa halmashauri zipatazo 60 tayari utekelezaji umeshafanyika katika awamu zilizopita na kwa sasa ni kwa wote, hili ni takwa la kisheria sio hiari.
Mafunzo haya kwa walengwa nikuongeza uwekaji wa akiba kidijitali, kujitambua na ujasiriamali, namna ya kukuza mtaji na kupunguza malalamiko toka kwa walengwa.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.