Aliyesimama ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mhe. Joseph G. Mandoo akifungua kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti Mhe. Petro Tarmo na Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Abubakar A. Kuuli.
Aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Sezaria V. Makota Akizungumza Katika Baraza Hilo
Wanaoonekana Wamevaa Majoho ni Waheshimiwa Madiwani Katika Kikao Hicho
Mhe. Calisti C. Casmiri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Toka Kata ya Bashay Ndiyo Makamu Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
Wanaoonekana Wamevaa Nguo za Kawaida ni Wakuu wa Idara, Vitengo na Wataalamu Wengine.
Wanaoonekana Hapo Juu ni Secretariati Ambapo Kushoto Ni Ndg. Honoratus Mulokozi na Kulia ni Ndg. Edes Melley.
Pakua bango kadhaa za kiao husika hapo chini:-
BARAZA MADIWANI 01.09.2022 FINAL 1.jpg
BARAZA MADIWANI 01.09.2022 FINAL 2.jpg
BARAZA MADIWANI 01.09.2022 FINAL 3.jpg
~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~
Haya yamejiri katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne ya mwaka wa fedha wa 2021/2022 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu tarehe 01.09.2022. Halmashauri ya Wilaya ya Mbuulu katika bajeti iliyoishia Juni 30, 2022 ilipanga kukusanya kiasi cha Tshs. 1,689,000,000.00 bilioni na kuweza kuvuka na kukusanya kiasi cha Tshs. 1,807,000,230.00 bilioni sawa na 107%. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Sezaria V. Makota amempongeza sana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Abubakar A. Kuuli pamoja na wataalamu wa halmashauri na baraza la waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mbulu Mhe. Joseph G. Mandoo kwa kuweza kutimiza vigezo vya OR-TAMISEMI kwa upande wa mapato na kupata cheti toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Charles M. Nyerere huu ni mwanzo mzuri utakaopelekea kuongeza kiwango cha utoaji wa mikopo kwa 10% ya makundi maalumu ya wanawake, vijana na walemavu lakini pia kuongeza ukubwa wa kiwango cha fedha zinazoenda kwenye miradi ya maendeleo kupitia vyanzo vya ndani kwa 40%.
Mhe. S.V.Makota katika taarifa zingine aliendelea kusema, katika zoezi la sensa linaloendelea hivi sasa katika dodoso kuu, kaya 41,585 sawa na 127.7% zilifikiwa hadi tarehe 31.08.2022 na katika dodoso la majengo hadi jana tulikuwa tumefika 133.5% na baadhi ya Kata zimeshamaliza lakini serikali imeongeza siku 7 kuanzia kesho tarehe 02.09.2022 ili tuweze kukamilisha maeneo ambayo hayakufikiwa hapo awali.
Katika umeme Meneja wa TANESCO Wilaya ya Mbulu anaenda kwa kasi inayotakiwa na kero zimepungua kwa kiasi kikubwa hasa baada ya kuwa karibu na wadau wa umeme ambao ni wananchi ambapo kikundi cha mtandao wa jamii wasap (wasap group) kimeundwa kwa nia njema ya kupeana habari za huduma ya nishati ya umeme kwa Wilaya na namna zinavyotatuliwa kwa wakati. Kwa wakandarasi wa maji nao wanakwenda vizuri sana na tunaendelea kufuatilia kama serikali kwa ukaribu ili kupata matokeo chanya katika miradi ya maendeleo. Kwa upande wa Wenyekiti wa Vitongoji walipangiwa kiasi cha Tshs. 50,000/= katika zoezi la sensa, hii inatia moyo tuipongeze serikali na hata sasa imeenda mbali zaidi kwa kutoa Tshs. 5000/= kila mwezi kwa kila Mwenyekiti wa Kitongoji kama fedha ya mawasiliano ambayo awali haikuwepo, ni pongezi kubwa sana kwa serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais wetu mpendwa, Mhe. Samia S. Hassan. Katika miradi vipolo Mhe. Makota ameagiza ikamilike kwa wakati kwani tumepewa hadi Oktoba 2022 iwe imekamilika lakini naimani hali itakuwa njema kwani maeneo mengi kama vile Endahagchan wanapambana kweli kweli kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati mradi wao.
Hata hivyo Mhe. Mkuu wa Wilaya alisema tujipange kwani ndani ya miezi michache ijayo kutoka sasa serikali inatarajia kutoa fedha za kujenga madarasa elfu 8 nchi nzima hivyo fedha zitakuja muda si mrefu kwa ajili ya miradi ya elimu, kwa hiyo tunaomba tupewe ushirikiano wa kukamilisha kwa wakati kama mradi wa vyumba vya madarasa ya UVIKO 19 yalivyofanikishwa kwa kishindo kwa halmashauri ya wilaya ya Mbulu. .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Mhe. Joseph G. Mandoo aliwashukuru sana, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbulu na timu ya wataalamu na waheshimiwa madiwani katika kumpa faraja na kufanikisha shughuli ya kumsindikiza mama mpendwa, mama mzazi wa Mhe. Mandoo aliyefariki jumatatu ya tarehe 22.08.2022 na kuzikwa ijumaa ya tarehe 26.08.2022 kwa niaba ya familia amefarijika sana, Mungu awabariki.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Mhe. Joseph G. Mandoo aliendelea kwa kusema, halmashauri tunapimwa katika nyanja nyingi ikiwamo namna ya kuwahudumia wananchi. Katika mapato tumevuka kwa 7% tujipongeze kwa hili itapelekea kuongeza kiwango cha fedha zinazokwenda kwenye miradi 40% na zile za makundi maalumu za 10%, lakini lazima tuende zaidi kwa kubaini fursa fiche, kuongeza vyanzo vipya na kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa utoroshaji wa mianya ya mapato ambazo kwa ujumla zitapelekea kukusanya zaidi.
Kimsingi serikali imeendelea kuleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo kama vile maji, barabara, afya na elimu bila kuchoka, kwa mwaka wa fedha unaoisha 2021/2022 tumepokea fedha za kupima viwanja kiasi cha Tshs.162 milioni, nyumba ya Mkurugenzi Tshs. 150 milioni, ukamilishaji wa jengo la Utawala Halmashauri ya Wilaya ya MbuluTshs. 2 bilioni , Tshs. 300 milioni kwa hospitali ya wilaya, shule mpya ya msingi kupitia mradi wa SEQUEP Tshs. 400 milioni na vituo 3 vya afya Maretadu, Haydom na Eshkesh kwa kweli hizi ni juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia S. Hassan kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na kuongeza kwa kusema "sisi twende kueleza yale mazuri ya serikali ya CCM kwa wananchi".
Hata hivyo, tumpongeze Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mhe. Flatei G. M kwa kuendelea kutupigania na kupata barabara ya lami, ambapo hadi sasa wakandarasi wako eneo la kazi (site) katika kipande cha kata ya Masqaroda wakiendelea na kazi, kwasababu itafungua fursa nyingi sana za kijamii na kiuchumi kwa wananchi, Mwisho Mhe. Mwenyekiti huyo alisisitiza wataalamu kuwa na nidhamu ili kutoa huduma bora kwa wananchi wote.
Katika kikao hiki kulifanyika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya Mhe. Petro S. Tarmo, Diwani wa Kata ya Masqaroda kumaliza muda wake, ambapo Mhe. Calisti C. Casmiri wa Chama cha Mapinduzi (CCM) toka Kata ya Bashay alipita bila kupingwa kwa kishindo cha kura zote 23 ambaye atahudumu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa mujibu wa kanuni Namba 4 na namba 1 ya uongozi wa ngazi hii kwa serikali za mitaa.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.