Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Chelestino Simbalimile Mofuga Akifungua Mafunzo ya Usajili na Kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto wa Umri Chini ya Miaka 5 Yaliyofanyika Katika Ukumbi wa Wanawake Mbulu Mjini Tarehe 07.05.2021
Katikati Aliyevaa Suti ni Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Chelestino Simbalimile Mofuga Katika Picha ya Pamoja na Wakufunzi wa Kitaifa na wa Wilaya ya Mbulu Katika Ukumbi wa Wanawake Mbulu Mjini Tarehe 07.05.2021
Katikati Aliyevaa Suti ni Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Chelestino Simbalimile Mofuga Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Baada ya Mafunzo Hayo Katika Ukumbi wa Wanawake Mbulu Mjini Tarehe 07.05.2021
Wanaoonekana Mbele ni Watumishi Hao Wakiwa Kwenye Mafunzo Kwa Vitendo Katika Ukumbi wa Wanawake Mbulu Mjini Tarehe 07.05.2021
Kulia Aliyevaa Shati Jeupe ni Afisa Ugavi wa Mbulu Bw. Edwin Akiwa Katika Zoezi la Kugawa Vifaa Kwenye Mafunzo Hayo Tayari kwa Kazi Katika Ukumbi wa Wanawake Mbulu Mjini Tarehe 07.05.2021
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Wakila Kiapo cha Utii na Kazi Kwenye Mafunzo Hayo Tayari kwa Kazi Katika Ukumbi wa Wanawake Mbulu Mjini Tarehe 07.05.2021
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~` TAARIFA KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Mofuga amewaasa watumishi wanaofundishwa kazi hii na kwenda kutekeleza kwa vitendo ni lazima wasikilize kwa umakini mafunzo yanayotolewa hapa na wataalamu wa "RITA" Taasisi ya inayoshugulikia usajili wa vizazi na vifo ngazi ya kitaifa na wale wa ngazi ya wilayana kauli mbiu ni "Mtoto anastahili cheti cha kuzaliwa mpe haki yake". Katika zoezi hili uwe mwadilifu katika kazi hii kwa kuzingatia kuwahi, kuwa na lugha nzuri na kujaza taarifa sahihi kwani lazima uwajibike kama ukienda kinyume na utaratibu zilizopangwa pia mwisho ni lazima tufanye kazi kwa uzalendo wa hali ya juu ili kutoa vyeti kwa watu sahihi.
Kwa Wilaya yetu wageni bado wamo kutokana na muingiliano wa masuala ya kiuchumi na biashara, andikisha mtoto aliyezaliwa Tanzania ili tusije tukapandikiza wageni. Cheti cha kuzaliwa ni utambulisho wa kwanza wa mtoto, kitamuwezesha mtoto kupata elimu na maisha bora na ni haki yake pia.
Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Mofuga aliongezea kuwa ukienda kufanya kazi kinyume na sheria kanuni na tararatu zilizowekwa tutashugulika na wewe. Hata hivyo mafunzo haya ni ya siku 3 kuanzia leo tarehe 07.05.2021 hadi 09.05.2021 ambapo baada ya hapa, tarehe 11.05.2021 mtaanza zoezi rasmi la usajili kwa Wilaya nzima kwa kwata zote 18 za Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa muda wa siku 12 hadi tarehe 22.05.2021 baada ya hapo ofisi ya Mkuu wa Wilaya itakuwa inaendelea kutoa vyeti hivi kwa utaratibu maalumu wa kulipia tofauti na sasa ni bure na serikali inagharamia kila kitu. Wananchi wengi hawapati vyeti sababu ya kuwa mbali na Wilaya lakini tukumbuke kuwa wenye umri zaidi ya miaka 5 sio wanufaika katika zoezi hili.
Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Mofuga ametoa angalizo na utekelezaji kwa kabila la wahadzabe ambao wanapatikana pia katika Wilaya ya Mbulu Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) Mbulu kwa kushirikiana na "RITA" ihakikishe inaangalia kwa jicho la tatu kwani hawa watu elimu ya kuwa na cheti cha kuzaliwa bado ni duni kwao, hivyo ametaka kuwepo utaratibu maalumu wa namna ya kutunza vyeti hivi kwa usalama zaidi.Mwisho amewashukuru wataalamu ngazi ya kitaifa kwa kuuleta mpango huu kwenye wilaya kongwe kama ya mbulu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.