Aliyeshika "MIC" ni Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt.Chelestino Simbalimile Mofuga Akifungua Mkutano wa Hadhara wa Wananchi wa Haydom
Aliyeshika "MIC" ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
Ndugu Hudson S. Kamoga Akisalimia Wananchi na Kumkaribisha Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu.
Aliyeshika "MIC" ni Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. C.S. Mofuga Kitoa Ufafanuzi wa Kero Mbalimbali Zilizotolewa na Wananchi wa Kata ya Haydom
Aliyeshika "MIC" ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson S. Kamoga kwa Nyakati Tofauti Akitoa Ufafanuzi wa Masuala Mbalimbali Yaliyojitokeza Katika Mkutano Huo.
Picha za Hapo Juu ni za Wataalamu Mbalimbali Wakuu wa Idara na Vitengo Pamoja na Watumishi Wengine wa Kiserikali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Katika Mkutano Huo.
Picha za Hapo Juu ni Baadhi ya Wananchi Waliouliza na Kutoa Maoni Mbalimbali Mbele ya Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt.Chelestino Simbalimile Mofuga Katika Mkutano Huo.
Aliyeshika "MIC" ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Haydom Ndugu Elihuruma Akijibu Maswali Yaliyoulizwa na Wananchi Katika Mkutano Huo.
Aliyeshika "MIC" ni Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Akitoa Ufafanua wa Masuala ya Ardhi Yaliyojitokeza Katika Mkutano Huo.
Aliyeshika "MIC" ni Mwakilishi wa Meneja wa Wakala wa Maji Mjini na Vijijini "RUWASA" Ndugu John Ombay Akitoa Ufafanua wa Masuala ya Maji Yaliyojitokeza Katika Mkutano Huo.
Aliyeshika "MIC" ni Meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini "TARURA" Nuru Hondo Akitoa Ufafanua wa Masuala ya Barabara Yaliyojitokeza Katika Mkutano Huo.
Picha za Hapo Juu ni za Wananchi Waliohudhuria Katika Mkutano Huo
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Hayo yamejiri leo katika mkutano mkuu wa hadhara wa wananchi wa kata ya Haydom ambapo mgeni rasmi alikua ni Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Mofuga. Dhumuni kubwa mkutano huu ni kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua ikiwa ni agizo la Mh.Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti baada ya kupata taarifa kuwa hawakuridhika na majibu ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu H.S.Kamoga pamoja na wakuu wa idara na vitengo katikamkutano mkuu wa hadhara wa tarehe 03.03.2021 uliosikiliza kero za wananchi na kuzitolea ufumbuzi wa uhakika.
Kimsingi mkutano wa leo ulikuwa wa manufaa chanya kwa wananchi wa haydom kwani kero mbalimbali za kisekta zilisikilizwa na kutolewa maamuzi hapo hapo zikiwemo za maji, barabara, elimu, ardhi na afya. Hata hivyo, wananchi wa Haydom katika mkutano huo wa hadhara mbele ya Mh. Mkuu wa Wilaya walimpongeza sana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson S. Kamoga kwa kuwa msikivu, mnyenyekevu na mwenye huruma kwa kila mwanachi kwa kusikiliza kero na kuzitolea ufafanuzi wa uhakika na ulioridhisha hivyo wapuuze kikundi cha watu wachache chenye nia mbaya ya kuvuruga maendeleo ya Haydom wakati wao si wakazi wa hapa Haydom.
Awali Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Chelestino Simbalimile Mofuga alitangulia kwa kuwauliuliza wananchi wa Haydom katika mkutano huo kama waliteua kikundi maalumu cha kwenda ngazi ya mkoa kuwasilisha kero zao badala ya kwenda ngazi ya Mkuu wa Wilaya baada ya wachache hao kudai kutoridhika na majibu ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu katika mkutano mkuu wa tarehe 03.03.2021 uliofanyika viwanja vya Ofisi ya Kata ya Haydom. Wananchi kwa kauli moja walijibu hatukuwatuma wala serikali ya kijiji hivyo wao ndio walioruka ngazi ya kwenda mkoani.
Hata hivyo, mgeni rasmi huyo alimpongeza sana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndugu Hudson S. Kamoga kwa kuwajali wananchi kwa kuja kuwasikiliza, kutoa ufafanuzi, miongozo na kutoa maamuzi juu ya kero zilizowasilishwa kwakekupitia mkutano huo.
Katika mjadala uliochukua takribani masaa zaidi ya 7 Mh.Mkuu wa Wilaya huyo alifikia maazimio haya ili kukamilisha utekelezwaji wa kero hizi.
Kwa vijiji vyote kila kijiji kuwe na na daftari la makazi ili kuwasajiri watu wote wanaoingia na kuishi Wilaya ya Mbulu ,pia mhusika ajulikane na serikali ya kijiji na mkutano mkuu kuwa katoka wapi na anafanya nini na kila gesti kwa kila mtu anayelala sharti arekodiwe kwenye daftari la wageni kwa usalama wa Wilaya yetu. Tunakaribisha watu mbalimbali kufanya biashara hapa lakini kwa kufuata taratibu za nchi yetu ili biashara ziendelee kufanyiaka bila wasiwasi.
Alimuagiza meneja wa Wakala wa Maji Mjini na Vijijini "RUWASA" kufanya hesabu za kitaalamu juu ya miradi ya maji ya Mbulu Mji na Haydom kisha kuileta katika kamati ya ulinzi na usalama.
Kuhusiana na maji, Meneja wa RUWASA ahakikishe kifaa cha kusukuma maji "motor" ikiharibika basi isizidi siku 5 iwe imerekebishwa na pia kama ni manunuzi yawe yameshafanyika kwani kukosa maji kutapelekea mlipuko wa magonjwa lakini pia hapa pana biashara pia zinazohitaji maji muda wote.
Meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini "TARURA" bwana Nuru Hondo alitamka kuwa wameshapokea karibu bilioni 1.2 mwaka huu ikiwa ni fedha za kujenga barabara za lami, za vumbi na mifereji yake kwa hiyo Haydom itapendeza.
Mkaguzi wa ndani ahakikishe anafanya ukaguzi wa kutosha katika kamati za wananchi za kupokea na kugawa chakula mashuleni kwa Wilaya nzima kisha kushauri njia itakayowawezesha kujiendesha kwa ufanisi na kupunguza migogoro isiyo ya lazima inayotookana na matumizi ya chakula husika.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.