Na Ruth Kyelula, Mbulu DC.
Miradi saba yenye thamani ya Bilioni 1,878,743,413 imefikiwa na mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara.
Hayo yalibainishwa mnamo tarehe October, 11, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu,Mkoani Manyara Kheri James, mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim.
Komred Kheri alisema Mwenge ulipokuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu umekimbizwa katika miradi saba yenye thamani ya Bilioni 1.8 na kukimbizwa katika umbali wa kilometa 100.3.
Aidha, alisema kati ya miradi 7, miradi mitatu imezinduliwa ambayo ni pamoja na mradi wa Maji Labay ambao umegharimu kiasi cha sh.1,069,270,393, ujenzi wa daraja la Barazani ambao umegharimu 249,980,000, na mradi wa Ujenzi wa shule mpya ya Msingi Flatei Massay iliyopo Haydom ambao gharama zake za ujenzi ni sh.348,500,000 kutoka serikali Kuu na nguvu ya wananchi ni milioni 17,500,000 ambapo inafanya jumlya yake kuwa Milioni 366,000,000.
“Pia Mwenge wetu wa Uhuru ukiwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu utafanya kazi ya kuona miradi miwili ambayo ni Uhifadhi wa chanzo cha maji Maghang, pamoja na kuona mradi wa karakana ya vijana ya kuchomelea vyuma,”Alisema Komred Kheri James.
Aidha Mwenge wa Uhuru ukiwa Halmashauri ya Wilaya hiyo, umefanya kazi ya kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ikiwa wa Ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Harsha pamoja na mradi wa Soko la mboga mboga uliopo katika kata ya Dongobesh.
Mkuu wa Wilaya alifafanua kuwa katika Utekelezaji wa miradi hiyo Serikali Kuu ilichangia jumla y ash. Bilioni 1,717,750,393, ambapo Halmashauri ya Wilaya hiyo imechangia miradi mitatu, Ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Harsha kwa kuchangia sh.Milioni 24.2, mradi wa karakana ya vijana ya kuchomelea vyuma kwa kuchangia sh.Milioni 5,554,445. Aidha alisema pia Halmashauri ya Wilaya imechangia katika ujenzi wa Soko la Mboga mboga kwa kuchangia sh. Milioni 93,948,375 na kupelekea jumla ya sh. Milioni 123,702,820.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Vijana CCM Taifa Komred Kawaida alisema kuwa yapo mambo mengi ya msingi na muhimu ambayo Mheshimiwa Raisi Dkt. Samia Suluhu Hasan anafanya kwa vijana wa kitanzania,ikiwemo mikopo ya asilimia 10, 4% kwa vijana, 4% kwa kinamama na 2% kwa watu wenye mahitaji maalumu lengo likiwa ni kujikwamua kiuchumi.
“Niwaambieni tunatambua mtihani tulionao sasa kwamba mikopo hii imesitishwa, niwatoeni hofu kuwa serikali inayo nia njema ya kuhakikisha mikopo hii inawafikia moja kwa moja walengwa ikiwa na maana kina mama, Vijana na Watu wenye mahitaji maalumu.”Alisema Kawaida.
Naye Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla Shaib Kaim amesema kuwa mbio za Mwenge za mwaka 2023 zimefika katika mradi wetu wa kikundi cha Vijana, kwanza kabisa Mwenge wa Uhuru kama ilivyokawaida tumepokea taarifa inayohusiana na mradi, tumefanya ukaguzi wa nyaraka, tumetembelea, tumekagua na kujionea shughuli ambazo kimsingi zinafanywa na vijana wetu.
"Ndugu zangu wapendwa niwaambie kwa dhati kabisa baada ya ukaguzi wa kina ambao tumefanya kwa upande wa nyaraka tumejiridhisha tumeona shughuli ambazo kimsingi vijana wetu wanafanya, tumeridhia shughuli wanazozifanya vijana wetu, nichukue fursa hii Mheshiwa Mkuu wa Wilaya na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa namna ya pekee mnavyoendelea kutoa mikopo hii kama programu ya kufuata na kutekeleza maagizo ya Serikali kwa lengo la kuwezesha wananchi kupitia programu ya 442, asilimia 4 Vijana, 4% Wanawake na 2% kwa watu wenye mahitaji maalumu. Hongereni sana kwa kazi mliyoifanya." Alisema Kaim.
Aidha Kaim alisema kuwa vijana wajitahidi kutumia fedha hizo kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama sehemu ya kujiajiri na kukuza kipato chao, pia amewashukuru vijana hao kwa kuwa wazalendo kwa kukamilisha marejesho ya mikopo yao . Amemuomba Mkuu wa Wilaya kuwasaidia vijana hao kupata mafunzo Ili bidhaa wanazotengeneza ziwe na ubora na viwango zaidi. Lakini pia muwasaidie katika upatikanaji wa tenda pamoja na mambo mengine.
#KWA PAMOJA TUNAIJENGA MBULU YETU
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.