Serikali imesaini Mkataba Ujenzi wa barabara ya Labay- Hydom kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilometa 25 , mradi huu mkubwa unagharimu zaidi ya blioni 40, ambapo utakapokamilika utarahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi kama vile usafirishaji wa mazao ya biashara na shughuli za kijamii kwa ujumla.
Mhandisi Godfrey Kasekenya
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi huo, iliyofanyika leo mei 19 .2023 katika viwanja vya Haydom Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara mgeni rasmi katika hafla hiyo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ameiagiza TANROADS kusimamia mradi huo kwa udhibiti mkubwa ili barabara iweze kutumika kwa muda uliopangwa
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila ametoa wito kwa mkandarasi kutekeleza mradi huo kwa weledi wa hali ya juu.
Aidha Mhandisi Kasekenya amesema Wilaya ya Mbulu inaenda kunufaika ujenzi mkubwa wa barabara tatu za lami zinazounganisha Mikoa mingine ya jirani.
Mbunge wa jimbo la mbulu Flatey Masey Ameishukuru serikali kupitia mradi huu uliosainiwa na kusema kilio cha muda mrefu kuhusu changamoto ya barabara hiyo kimeisha na hivyo wananchi wao wamejipanga tayari kutumia fursa ya ujenzi wa barabara hiyo
Mbunge wa Mbulu Flatey Masey
KWA PAMOJA TUNAIJENGA MBULU YETU
WANANCHI WA HAYDOM
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.