Mpango wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuendelea kufanya upanuzi wa mkongo wa Taifa ili kuimarisha mawasiliano na kujenga jamii habari nchini,hatimae umeifikia wilaya ya Mbulu.
Katika mpango huo wa Serikali,wilaya ya Mbulu itakuwa miongoni mwa wilaya zitakazo fikishiwa Mkongo wa Taifa wa mawasiliano ili kurahisisha huduma za mawasiliano ya simu,huduma za malipo katika mitandao na taasisi za fedha,huduma za redio na Televisheni,pamoja na elimu mtandao.
Akizungumza katika kikao maalumu cha uwasilishaji wa taarifa rasmi ya kuanza kwa ujenzi huo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Mbulu,Meneja wa huduma kwa wateja kutoka TTCL ndugu Wendlyne Mbagga pamoja na ndugu Edson Richard kutoka ofisi ya Mkongo wa Taifa,wameeleza kuwa ufikishwaji huo wa huduma za mkongo katika wilaya ya Mbulu,utakwenda sambamba na ujenzi wa kituo cha huduma kitakacho jengwa Mbulu Mjini.
Akizungumza katika kikao hicho maalumu cha kuutambulisha mradi,Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James amemshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi huo muhimu unaolenga kuboresha maisha ya wananchi na kurahisisha huduma katika jamii.
Komred Kheri James amesema kuwa Serikali katika wilaya ya Mbulu imejipanga kuusimamia mradi huo vyema,na kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotarajiwa ili kukidhi malengo ya huduma kwa wananchi.
Mkongo wa Taifa unatumika kutoa huduma za kisasa za utumaji na upokeaji wa Taarifa,pamoja na utoaji wa huduma za afya mtandao (e-health),Elimu mtandao (e-learning),Serikali mtandao (e-government) na huduma zingine nyingi za kiuchumi na kijamii.
Maandalizi ya ujenzi wa upanuzi huo wa Mkongo kwa wilaya ya Mbulu yako tayari,na wakati wowote kuanzia sasa Mkandarasi ataanza utekelezaji wa mradi huo muhimu kwa wananchi.
#Kwapamoja, Tunaijenga Mbulu yetu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.