Dongobesh 17/07/2023
Mkurugenzi Mtendaji ndugu Abubakar Kuuli hii leo ameongoza kikao cha tahimini ya hali ya lishe kwa kipinidi cha aprili hadi juni 2023 katika ukumbi wa vikao vya halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kilichoshirikisha Wataalam ngazi ya Wilaya na wataalam kutoka Idara ya Afya.
Akisoma taarifa ya hali ya lishe ndugu Martin Mwandiki( Mganga Mkuu wa Wilaya), amesema tuna jumla ya vituo 31 vya kutolea huduma za Afya,kati ya vituo hivyo , vituo vitatu(3) vya Dongobesh,Hyadom na St. Aloisi vinatoa huduma ya matibabu ya utapia mlo mkali wodini kwa watoto waliolazwa na kueleza hatua zinazoendelea kuchukuliwa ili kutokomeza hali hii.
Aidha ameeleza shughuli mbalimbali zimeendelea kufanywa ikiwa ni pamoja na otuaji wa matone ya Vitamini A watoto chini ya miaka mitano,uchunguzi wa hali ya lishe, utoaji wa madini chuma kwa akina mama wajawzito, elimu ya lishe na utoaji wa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
Akiongea kwa upande wa lishe Bi. Jackline ambaye ni Afisa lishe wa Wilaya, amesema tumefanikiwa kutoa lishe kwa asilimia mia, aidha tunaendelea kutoa elimu ya lishe na mapishi darasa kwa ngazi ya vijiji,na kuendelea kutoa elimu juu ya uandaaji wa lishe bora kwa watoto.
“Niwatake wataalam wa Afya kuhakikisha hatulali na tunazunguka katika vijiji vyote, mashuleni na vituo vya kutolea huduma mkishirikiana na Watendaji katika kupambana na kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa lishe bora na namna ya uandaaji wa chakula bora cha lishe kwa watoto wote walio chini ya miaka mitano”. Alisema hayo Mkurugenzi alipokuwa akihitimisha kikao hicho.
"KWA PAMOJA TUNAIJENGA MBULU YETU"
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.