Ndugu Abubakari Kuuli Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu akiweka udongo wakati wa usimikaji wa Nguzo za barabara
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndugu Abubakari Kuuli leo ameongoza zoezi la usimikaji wa Nguzo za barabara ili kuweza kuonesha uelekeo wa barabara ikiwa ni utekelezaji wa zoezi la anwani na Makazi linaloendelea katika Halmashauri hiyo.
ndugu Horace Kolimba akiwa na furaha mara baada yakuona kibao cha barabara kilichosimikwa katika mji wa Dongobesh
Kutoka kushoto ni Ndugu Sadoth Kyaruzi Mratibu wa NaPa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Ndugu Abubakari Kuuli (Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu) na Ndugu Horace Kolimba (Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu0 kwa Pamoja wakifurahi mara baada ya zoezi la usimikaji wa nguzo za barabarabara kukamilika
Ndugu Kuuli amempongeza Mratibu wa zoezi hilo ndugu Sadoth Kyaruzi kusimamia vizuri zoezi hilo kwa kushirikiana na timu yake ya Napa na kufanikisha usimikaji wa nguzo zaidi ya 20 katika Mji wa Dongobesh, amemuomba kuendelea na zoezi hilo mpaka ifikapo tarehe 30/05/2022 hakikishe maenomengine ya kiutwala yaliyobaki yawe yamewekewa nguzo zote za Mtaa pamoja na vibao vya nyumba na Makazi vimekamilika.
moja ya nguzo ya barabara ikionesha mtaa husika
Aidha baadhi ya Wananchi wa Mji wa Dongobesh wakiongoza na Mhe. Joseph Barabojick (Diwani wa kata ) wameishukuru Serikali kwa kuleta utaratibu wa utambuzi wa maeneo hasa katika mji huo unao kuwa kwa kasi na hii ikiwa ni mara baada ya kuhamishia Makao Makuu ya Halmshauri na kuweza kusadidia hata kwa mgeni aingiapo katika Mji huo anaweza kujionea ni kwa jinsi gani ulivyopangika na ukiwa na alama za barabara kama jinsi nguzo hizo zinavyoonesha maeneo mbalimbali.
Mhe. Joseph Barabojick Diwani wa kata ya Dongobesh akisoma kwa makini jina la Mtaa lililoandikwa katika moja ya nguzo zilizo simikwa
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.