Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Anayeondoka wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini Ndugu, Hudson S. Kamoga na Kulia ni Mkurugenzi Mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini Ndugu, Abubakar Abdullah Kuuli na Katikati ni Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini, Mandoo Wakiwa Katika Shuguli ya Makabidhiano.
Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini, Joseph Mandoo Akisaini Nyaraka za Makabidhiano.
Mtunza Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini, Ndugu R. Kagaruki Akisaini Nyaraka za Makabidhiano.
Mkurugenzi Mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini Ndugu, Abubakar Abdullah Kuuli Akizungumza Katika Makabidhiano Hayo
Picha Mbalimbali za Wataalam Katika Makabidhiano Hayo
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Haya yamejiri leo katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijiji mbele ya wakuu wa Idara na vitengo na baadhi ya watumishi wengine. Katika makabidhiano hayo walihudhuria pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini Mh. Mandoo na Makamu wake.
Mkurugenzi anayeondoka amefanya mengi kwa kadri alivyoweza kwa kushirikiana na baraza la madiwani na wataalam wa halmashauri katika kufanikisha jukumu kubwa la kuwaletea maendeleo wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini.
Katika kipindi chote cha miaka mitano Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imeendelea kupata hati safi, ongezeko la utoaji wa fedha za makundi maalimu ya wanawake vijana na walemavu kutoka asilimia 0 mwaka 2015 hadi asiliamia 102 kwa miaka ya karibuni. kuongezeka kwa mapato ya halmashauri hadi kufikia shiling bilioni 1.35 kulikopelekea kuongeza kasi ya kutatua kero mbalimbali zikiwemo za watumishi.
Mwisho ndugu. Kamoga amewashukuru watumishi wote na waheshimiwa madiwani kwa kuwa naye bega kwa bega katika kushirikiana kwenye kazi hii ngumu tangu alipoingia hadi sasa. Ameomba pande zote kushikrikiana ili kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbul Vijijini. Hata hivyo ameomba pale alipokwaza asamehewe kwani ilikuwa ni katika hali ya kutekeleza majukumu ya kiserikali naye pia amesamehe kwa mambo mbalimbali yaliyopita.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mh. Mandoo alisisitiza kwa kusema tushirikiane vizuri na Mkurugenzi kwa kumpa ushauri wenye tija, tujitume katika kazi na kila atakaloambiwa na mtu yeyote kwa hapa Mbulu basi achuje kwa umakini sana kujua ukweli kabla ya kufanya maamuzi.
Mkurugenzi mpya ndugu, Abubakar Abdullah Kuuli amesisitiza kwamba ataweka kipaumbele kwa nguvu na ari katika sehemu za ukusanyaji wa mapato, matumizi ya mapato ya ndani katika makundi maalumu yaani wanawake, vijana na walemavu kwa kusikiliza na kutatua kero za wananchi, kusimamia miradi ya maendeleo ili kuhakikisha inakamilika kwa muda mwafaka na kwa kiwango cha juu. Aliendelea kwa kusema uwepo na kauli nzuri kwa watumshi katika kuwahudumia watumishi wenzao na wananchi kwa ujumla, mwisho kufanya kazi kwa weledi kwa kila mtaalam.
Hivyo basi, kama wakuu wa idara na vitengo tukashirikiana vizuri, madiwani wakishirikiana vizuri na pia menejimenti ikishirikiana na baraza la waheshimiwa madiwani vizuri kila kitu kitakuwa rahisi na hakika tutafikia malengo tuliyojiwekea. Bado halmashauri ya wilaya ya mbulu ina changamoto za watumishi kama ilivyo katika halmashauri zingine hususan Idara ya Ujenzi, Ugavi, Utawala na Afya, tunaimani serikali itaendelea kusikiliza kilio hiki na kuleta watumishi.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.