DOdoma
Mkurugeniz msaidizi wa mifumo ya TEHAMA-OR TAMISEMI ndugu Baltazari Kibola, amfungua mafunzo rasmi leo katika ukumbi wa mafuzo Epicor dodoma, akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi amewaomba washiriki kuwa makini kuzingatia mafunzo yatakayotolewa na wawwezeshaji.
akizungumza mbele ya washiriki 27,kutoka halmashauri 17 wanaowawakilisha Maafisa TEHAMA na Wahasibu wa Mapato amewaomba washiriki hao kuwa makini ili kuweza kupata mafunzo yatakayowasaidia pindi warudipo kwenye vituo vyao vya kazi waweze kutatua kwa umakini changamoto zinazowakabili kupitia mfumo wa Mapato (LGRCIS)
MKURUGENZI MSAIDIZI WA MIFUMO YA TEHAMA NDUGU BALTAZAR KIBOLA(aliyesimama) akiwa ameambatana na MRATIBU WA MFUMO WA MAPATO NDUGU MANDA(wa kaza kushoto) pamoja na mwenyekiti wa washirik wakimsikiliza mwenyekeiti
Aidha Mkurungezi Msaidizi amewaomba washiriki kuonesha ushirikiano ili kuweza kusaidia Halmshauri kutatua changamoto zinazojitokeza mara kwa mara kwenye mfumo, na hii ndio sababu kuombwa na Wakurugenzi kushiriki katika mafunzo hayo siku ya leo. akisisitiza mafunzo haya amewaomba washiriki kuwa makini zaidi kuzingatia mambo yafuatayo:-
usimamizi na matumizi sahihi ya vifaa vya kukusanyia Mapato (POS)
Kuzingatia mgawanyo wa majukumu kwa watumiaji wa mfumo wa mapato kwa kuzingatia kada ya Afisa TEHAMA,Afisa Mapato,Cashier,Afisa biashara na Mwekahazina
Kuepuka utengenzaji wa bill mbili mbili hasa wakati wakutengeneza bill kwenye kipengele cha miscellaneous
Kubaini makosa yanayofanywa kwa kukusudia au bahati mbaya na mkusanya mapato
Kuwa makini zaidi katika kusajili mashine za kukusanyia mapato ili kuweza kuepuka ukusanyaji wa chanzo kimoja kuingilia na chanzo kingine
BAADHI YA WASHIRIKI WAKIMSIKILIZA MKURUGENZI MSAIDIZI WAKATI WA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA MFUMO WA MAPATO
washiriki toka halmashauri mbalimbali wakiendelea kusikia ushauri kutoka kwa Mkurugenzi wakati wa ufunguzi wa mafunzo
Afisa TEHAMA kutoka muheza,ambaye pia ni katibu akionesha sura ya tabasamu mara baada ya kupitia mfumo
Afisa TEHAMA kutoka halmshauri ya Babati (wa kwanza kulia)akiwa na Afisa Mapato kutoka halmshauri ya Wilaya Mbulu kwaiendelea kupitia mfumo wa mapato
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.