Akitembela majeruhi hao Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndugu Abubakar Kuuli amewajulia hali na kutoa pole kwa majeruhi wote waliolazwa katika kituo cha afya Dongobesh.
Ajali hiyo imetokea hii leo tarehe 07/08/2023,mnamo majira ya saa 10 jioni kwa Basi la abiria Kampuni ya Bashnet Coach yenye usajili wa namba T 873 BMX inayofanya safari zake za kila siku kati ya Mbulu- Dongobesh-Babati katika Mlima wa Qaloda na basi hilo kushindwa kutokana na hitilafu ndogo.
Katika ajali hiyo Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Dokta Martin amethibitisha kutokea kifo cha mtu mmoja mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Hassan Ramadhani mkazi wa Kondoa,majeruhi 21 kati yao ni Wanaume 05, wananwake 15 na mtoto 1 wamepokelewa na kulazwa katika kituo cha Afya Dongobesh uku wakiendelea kupata matibabu katika kituo hicho na hospitali ya Wilaya.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.