Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. A. A. Kuuli Akikabidhi Vifaa Hivyo Kama Inavyoonekana Kwenye Picha Hapo Juu, wa Kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Yaeda Chini Bi. Tatu Ismail.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. A. A. Kuuli Akipokea Taarifa ya Mgao kwa Vijiji Hivi 2, Kutoka Kulia ni Afisa Malalamiko Wilaya ya Mbulu Bw. Edes Marlley Katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) Dongobesh - Mbulu.
Vifaa Husika Mikeka 10, Vikombe Vikubwa 10, Masufuria ya Wastani 10, na Galoni za Maji za Lita 10, 10
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. A. A. Kuuli Akikabidhi Vifaa Hivyo Kama Inavyoonekana Kwenye Picha Hapo Juu, wa Kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Yaeda Chini Bi. Tatu Ismail.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. A. A. Kuuli Akikabidhi Vifaa Hivyo Kama Inavyoonekana Kwenye Picha Hapo Juu, wa Kushoto ni Mh. Faustine Fisoo ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Qedesh.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. A. A. Kuuli Akizungumza Katika Makabidhiano Hayo.
~~~~~~~~~~ HABARI KWA UNDANI ~~~~~~~~~~
Haya yamejiri leo baada ya Mkurugenzi Mtendaji (W) kukabidhi mikeka kwa kila kijiji kwa vijiji hivi viwili kwa idadi ya mikeka 5, masufuria 5, vikombe vikubwa 5 na Magaloni ya maji ya lita kumi 5 kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa kwa lengo la kuwakabidhi watu waliopata maafa katika maeneo yao. Waliopokea kwa niaba ya wananchi ni Tatu Ismaili ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Yaeda Chini Afisa mTendaji wa Kijiji cha Dongobesh Chini Bw. Emanuel Baynit wakiwa na Mh. Faustine Fisoo ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Qedesh.
Mnamo mwezi Agosti 2021 mwananachi aitwae Julius Haqwe wa kitongoji cha Qedesh Kijiji cha Dongobesh Chini, Kata ya Dongobesh alipatwa majanga ya kuunguliwa nyumba ya makazi yake na moto uliozuka ghafla kwenye nyumba yake na kuteketeza mali zote zilizokuwa katika nyumba hiyo ikiwa ni pamoja na vyombo mbalimbali vya matumizi ya nyumbani, nguo, nafaka na vingine vingi.
Baada ya hali hii kujitokeza kijiji waliweka mkutano mkuu wakaelezwa ndipo siku iliyofuata wananchi walijikusanya kupitia kamati zao za kijamii na kumsaidia yule mama kwa kumpa hifadhi na kujengewa nyumba nyingine na kumsaidia mahitaji mbalimbali ya msingi ambapo hadi sasa anaendelea vizuti.
Mnamo mwezi Agosti 2021 kwa mara nyingine tena katika Kijiji kingine Wilaya hii hii ya Mbulu Vijijini mwananachi aitwae Rozalia Qella wa kitongoji cha Laghanga Kijiji cha Yaeda Chini, Kata ya Yaeda chini alipatwa majanga ya kuunguliwa nyumba ya makazi yake na moto uliozuka ghafla kwenye nyumba yake na kuteketeza mali zote zilizokuwa katika nyumba hiyo ikiwa ni pamoja na vyombo mbalimbali vya matumizi ya nyumbani, nguo, nafaka, kuku2 na mbuzi 2.
Baada ya hali hii kujitokeza kijiji waliweka mkutano mkuu wakaelezwa kisha siku iliyofuata wananchi walijikusanya kupitia kamati zao za kijamii na kumsaidia yule mama kwa kumpa hifadhi na kujengewa nyumba nyingine na kumsaidia mahitaji mbalimbali ya msingi ikiwemo chakula debe 3, fedha za Serikali ya Kijiji Tsh. 200,000/= na wananchi walichanga Tsh. 76,000/= ambapo hadi sasa anaendelea vizuri.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji (W) huyo, ameishukuru Serikali kwa kutoa vifaa hivi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwani vitasaidia wananchi pindi maafa yanapojitokeza kama hivi leo. Pia Mkurugenzi huyo amesisitiza Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji (WEO na VEO) wawe wanatoa taarifa hizi mapema ili kama ni misaada basi itoke kwa wakati ili kutimiza lengo la huu msaada wa maafa kwa walengwa.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.