Kutoka Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii (W), Bw. Sulle wa pili ni Mkurugenzi Mtendaji (W) Bw. A. A. Kuuli na wa tatu ni Mh. Diwani Viti Maalu (CCM), Shishi Katika Kikao Hicho.
~~~~~~~~~HABARI KAMILI~~~~~~~~~~
Mkurugenzi huyo aliongozana na kamati ya uhamasishaji ambayo ilikuwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Sulle na wengine wengi, hata hivyo alikuwepo Mh. Diwani wa wa Viti Maalumu kutoka Kata ya Tumati.
Kutembelea katika sehemu hizi kwa Mkurugenzi Mtendaji (W) Bw. A. Kuuli kunamfanya aweze kujua na kutatua changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza hivyo atakuwa na uwezo wa kuzitatua kwa haraka zaidi kuliko angekuwa ofisini. Katika miradi hii kata ya Tumati imepokea kiasi cha Tsh Milioni 40 ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 2 shule ya sekondari Endoji Kata ya Tumati ambapo kupitia kikao hicho viongozi na wawakilishi wa wananchi wamekunbaliana kuupokea huo mradi kisha kuushusha kwa wananchi na kuanza taratibu za uundaji wa kamati za usimamizi wa mradi huo na kuanza zoezi la usafi katika eneo la kazi kesho tarehe 02.11.2021. Pia zoezi hili litaambatana na wananchi kuanza kuleta malighafi za ujenzi zinazopatikana katika maeneo yao ikiwemo mchanga, mawe na kokoto.
Tumati ni moja wapo ya Kata iliyopokea kiasi cha fedha hizo toka Serikali kuu kupitia fedha za mpango wa UVIKO 19 zilizotolewa na muongozo toka OR-TAMISEMI na ukamilishaji wake ni miezi 2 ijayo kutoka sasa ili kuhakikisha watoto wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2022 kutokukosa nafasi. Kata ya Tumati ina vijiji 5 ammbavyo ni Tumati, Mongahay, Endoji, Getesh na Endesh
.
Kikao cha aina hiyo hiyo kimefanyika Kata ya Dongobesh leo tarehe 01.11.2021 kwa kazi hizo hizo lakini tofauti yake ni kwamba Shule ya Sekondari ya Alexanda Saulo imepokea kiasi cha Tsh. milioni 60 ambazo kwa mujibu wa muongozo zitajenga vyumba vya madarasa 3. Kata ya Dongobesh ina vijiji 3 ambavyo ni Dongobesh chini, Dongobesh na Qaloda.
Hata hivyo kupitia kikao hicho viongozi na wawakilishi wa wananchi wamekunbaliana kuupokea huo mradi kisha kuushusha kwa wananchi na kuanza taratibu za uundaji wa kamati za usimamizi wa mradi huo na kuanza zoezi la usafi katika eneo la kazi kesho tarehe 02.11.2021. Pia zoezi hili litaambatana na wananchi kuanza kuleta malighafi za ujenzi zinazopatikana katika maeneo yao ikiwemo mchanga, mawe na kokoto.
Kimsingi wananchi wote wamefurahi sana baada ya kupata taarifa hizi njema kwa watoto wao na kuishukuru sana serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Mh.Rais. Samia S.H. kwa kuwaletea fedha hizi kwa ajili ya watoto wao kuendelea na masomo bila shida Januari 2022.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.