Kutoka Kushoto wa Pili ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw.Abubakar A. Kuuli Akiwa na Timu ya Wataalamu (CMT) Wakikagua Mradi wa Viwanja Dongobesh Mjini
Mkuu wa Idara ya Ardhi Bw. Finias Kagenda (wa katikati aliyevaa koti jeusi) Akitoa Ufafanuzi wa Viwanja Hivyo kwa Kufuata Michoro na Ramani za Mipango Miji
~~~~~~~~~~~~ HABARI KWA UFUPI ~~~~~~~~~~~~
Mkurugenzi Mtendaji huyo Bw. A. Kuuli alikagua utekelezaji wa mradi huo akiwa na timu ya wataalamu (CMT). Mradi huu wa Viwanja vya Dongobesh Mjini ambao kwa sasa uko katika hatua za awali lakini baada ya taratibu mbalimbali kukamilika basi wananchi na wadau mbalimbali watapewa taarifa rasmi ya kununua viwanja hivyo, ambapo kwa halmashauri ni njia moja wapo ya kuongeza mapato lakini katika mipango miji Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Mbulu imefanya jambo la msingi sana kwa ajili ya kuupanga mji kwa miaka mingi ijayo. Ambapo ufikaji wa kila eneo unakuwa ni wa uhakika kwa kila aina ya miundombinu na utoaji huduma mtambuka kwa wakazi wa eneo husika.
Hata hivyo katika kuhakikisha viwanja vinaoneka katika kila eneo kilipo na kurahisisha upitishaji wa miundombinu muhimu ya maji na umeme tayari kazi ya uchongaji wa barabara unaendelea ambapo zoezi hili limeanza tarehe 12.11.2021 na linatarajia kukamilika tarehe 17.11.2021
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.