Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson S. Kamoga Akizungumza na Watumishi Katika Mafunzo ya Usajili na Kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto Chini ya Umri wa Miaka 5 Kwenye Ukumbi wa Wananwake Mbulu Mjini Leo Tarehe 08.05.2021
Picha za Hapo Chini Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Wakiwa Katika Mafunzo ya Usajili na Kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto Chini ya Umri wa Miaka 5 Kwenye Ukumbi wa Wananwake Mbulu Mjini Leo Tarehe 08.05.2021
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~` TAARIFA KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson S. Kamoga amesisitiza kufanya kazi kwa weledi kwa watumishi wanaofundishwa mafunzo ya usajili na utoaji vyeti kwa watoto chini ya umri wa miaka 5 yanayotolewa na wataalamu ngazi ya Wilaya kwa ushirikiano na wataalamu wa ngazi ya kitaifa yaani "RITA" Taasisi ya inayoshugulikia usajili wa vizazi na vifo kauli mbiu ni "Mtoto anastahili cheti cha kuzaliwa mpe haki yake".
Katika zoezi hili Mkurugenzi Mtendaji amesisitiza kuzingati sheria kanuni na taratibu za kazi husika ili kuweza kufikia malengo na kutoingiza dosari kwa mtumishi yeyote ambaye yupo kwenye zoezi hili. aliendelendelea kwa kusema uadilifu katika kazi,kuzingatia kuwahi kazini, kuwa na lugha nzuri na kujaza taarifa sahihi kwani hasa ukizingatia majina ya wananchi wetu inatakiwa usikilize vizuri ndiyo uelewe lasivyo utaandika kitu ambacho hakipo mfano jina tlatla usiposikiliza vizuri utaandika tata.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imejiandaa vilivyo katika zoezi hili la kitaifa ikiwa ni pamoja na kutoa matangazo ya hamasa kupitia Radio,mbao za matangazo kwenye kata na vijiji, mikutano ya vijiji, kutangaza kupitia gali maalumu la matangazo la halmashauri katika kata na vijiji vyote pamoja na tovuti ya halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ili wananchi wapate nafasi hii muhimu ya kusajiri watoto wao.
Mkurugenzi Mtendaji ameishukuru serikali kwa zoezi hili muhimu litakalowasaidia watoto hawa hadi uzee wao katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kibiashara, kiserikali na kimaisha kwa ujumla wao. Hata hivyo imewaondolea adha wananchi ambao walikuwa mbali na uwezo mdogo wa kupata cheti hiki kwani ni bure na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo inayogharamia zoezi hili kwa masalahi mapana ya nchi yetu na wanachi wake.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.