Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar Abdallah Kuuli, Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Bw. Furaha Simbeye na wa Kulia Mwisho ni Afisa Elimu Bw. Niela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar Abdallah Kuuli Akiwa na Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Bw. Furaha Simbeye Wakielekea Kwenye Mradi wa Bweni Katika Shule ya Sekondari ya Dr.Olsen Iliyopo Kata ya Haydom.
Picha za Hapo Juu ni Muonekano wa Bweni Lililokamilika Shule ya Sekondari ya Dr.Olsen Iliyopo Kata ya Haydom Linauwezo wa Kuchukua Zaidi ya Wanafunzi 80.
Picha za Hapo Juu ni Muonekano wa Mradi wa Ujenzi wa Vyumba 2 Vya Madarasa na Ofisi Moja ya Waalimu Unaoendelea Kukamilishwa Katika Shule ya Sekondari ya Dr.Olsen Iliyopo Kata ya Haydom.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. A. A.Kuuli Akiwa na Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Bw. F.Simbeye Akitoa Maelezo Juu ya Sehemu ya Kuzalishia Vyura Kwa Ajili ya Mafunzo Kwa Vitendo Kwa Wanafunzi wa Mchepuo wa Sayansi Katika Shule ya Sekondari ya Dr.Olsen Iliyopo Kata ya Haydom.
Katikati Kwenye Picha za Hapo Juu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. A. A.Kuuli Akiwa na Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Bw. F.Simbeye Kulia Wakiwa na Waalimu wa Shule ya Sekondari ya Dr.Olsen Iliyopo Kata ya Haydom.
Picha za Hapo Juu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. A. A. Kuuli Akiwa Akiwa na Mwalimu Wariamboro Saulo (katikati) na Mwalimu Agnes Mtweve (kushoto) Wakielekea Kwenye Mradi wa Vyumba Vya Madarasa 2 Katika Shule ya Msingi Haydom Iliyopo Kata ya Haydom.
Jengo la Madarasa 2 na Ofisi 1 ya Waalimu Katika Shule ya Msingi Haydom Iliyopo Kata ya Haydom Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Katika kuhakikisha kero za wananchi zinatatuliwa katika sekta mbalimbali kupitia ukamilishaji wa miradi mtambuka ya maendeleo Mkurugenzi Mtendaji Bw. A.A.Kuuli katika ukaguzi huo wa miradi ya elimu Kata ya Haydom amewataka waalimu na kamati zote za miradi ngazi ya kata na vijiji kusimamia kwa umakini mkubwa kiasi kwamba thamani ya fedha iakisi ubora wa mradi husika kwani mradi ukiwa mzuri na wananchi hawatahangaika kurudia tena ujenzi, huku muda nao ukitakiwa kuzingatiwa kwa kwenda na kasi inayostahili ili kero za elimu ziweze kutokomezwa.
Hata hivyo katika baadhi ya miradi aliyoikagua moja wapo ni ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa Shule ya Sekondari Dr.Olsen kwa gharama ya Tsh. 40,000,000/= iliyopokelewa kutoka serikali kuu katika Kata ya Haydom, ambayo ujenzi wake ulianza mwanzoni mwa mwezi Agosti 2021 na sasa iko katika hatua ya ukamilishaji wa vitu vichache kama vile rangi na vingine vidogo vidogo unaendelea vizuri kwa mujibu wa Mwalimu aliyekutwa maeneo ya kazi.
Kwa wakati huo huo shule ya Msingi Haydom Kata ya Haydom Mkurugenzi Mtendaji Bw. A.A.Kuuli amekagua pia ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa kwa gharama ya Tsh. 40,000,000/= iliyopokelewa toka serikali kuu, ambapo hadi sasa hatua iliyofikiwa ya kimaumbile ni ukamilishaji wa baadhi ya vitu vidogo vidogo ili wanafunzi waanze kuyatumia.
Ili kuweka mazingira wezeshi kwa watumishi ambao ni waalimu kila jengo la lenye vyumba vya madarasa 2 basi ni lazima pawepo na ofisi 1 ya waalimu kwa gharama ile ile hili ni jambo la kuigwa na la busara mno ambalo limetokana na uongozi mzuri wa kimkakati wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) Kwa fedha za wananchi na Serikali yao ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uimarishaji wa mabweni ya wanafunzi kutasaidia kupunguza mimba kwa watoto wa shule, utoro wa wanafunzi, kupungua kwa kupoteza muda mwingi wa wanafunzi kutembea wakati wa kurudi kwa wazazi wao hii itapelekea matokeo chanya ya tabia njema na kuongezeka kwa ufaulu wa wastani wa daraja la juu kwa wanafunzi wengi hususani wakike. Bweni hili lililokaguliwa leo limetumia gharama ya Tsh. 80,000,000/= na litaanza kutumika muda si mrefu kwa kuwa na uwezo wa kuhifazi wanafunzi wasiopungua 80 kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw.Furaha Simbeye.
Mkurugenzi huyu amewapongeza waalimu, kamati husika na Idara ya Ujenzi kwa kuchapa kazi nzuri hivyo waendelee na kasi zaidi kwa hali hii itasaidia kupandisha ufaulu wa watoto ambao baadaye watakuja kuisaidia jamii husika.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.