Na Magreth Mbawala,Mbulu DC
Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Mbulu limepitisha kiasi cha shilingi bilioni 38,747,893,000 kama bajeti kwa kipindi cha mwaka 2025/2026.kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo na mishahara.
Mapendekezo hayo yalifanyika katika mkutano wa baraza la madiwani wakati wa kupitisha bajeti ya mwaka 2025/26 ambayo yalifanyika tarehe 13/2/2025 katika ukumbi wa Halmashauri.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu Mh Joseph Mandoo alisema kuwa kupitia vikao vya kamati mbalimbali za madiwani walikubaliana bajeti hii itawapa vipaumbele kata ambazo bado hawajafikiwa na miradi mikubwa ili kuongeza chachu kwa wananchi.
Sambamba na hilo Mh Mandoo alisema bajeti ya makusanyo ya ndani kwa waka huu wa fedha ni shilingi bilioni 3.5 hivyo ni jukumu la kila mmoja kuwajibika,kusimamia na kuhakikisha fedha hizo zinapatikana na kuendeleza rekodi ya kuwa kinara kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani kwenye halmashauri za mkoa wa Manyara.
Pia Mh Mwenyekiti alikumbusha kuwekwa kwa bajeti ya motisha ya walimu kwa shule ambazo zitafanya vizuri kwenye halmashauri maana ni jambo ambalo walishakubaliana ,Kwakufanya hivyo itaongeza ufaulu kwenye shule na ushindani utaongezeka.
Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia Baraza la Bajeti, Februari 13, 2025.
Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu Abubakar Kuuli alisema kuwa bajeti ya mwaka huu wa fedha kwa mapato ya ndani ni bilioni 3.5 ambapo hadi kufikia mwezi huu wa pili tayari bilioni 2 zimeshakusanywa na wanatarajia watavuka malengo hayo kama ilivyokuwa desturi yao.
Wataalamu na kamati ya Ulinzi na usalama wa Wiaya, wakifuatilia Baraza la Bajeti.
Mkurugenzi aliendelea kumshukuru Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapa fungu kwenye bajeti ambayo inachangia uendeshaji wa halmashauri kwa kiasi kikubwa kwani bila fungu hilo wao kama halmashauri wangeweza kujiendesha kwa siku 33 tu ndani ya mwaka mzima.
Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Bajeti , Februari 13, 2025
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.