Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. C.M.Nyerere Katika Kikao cha Hoja za CAG Kilichofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu - Dongobesh,
Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mhe. Joseph G. Mandoo
Waheshimiwa Madiwani
Wataalamu Mbalimbali
~~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~
Haya yamejiri leo tarehe 24.06.2022 katika kikao maalumu cha Hoja za CAG ambacho Mwenyekiti wa kikao hicho ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Makongoro Nyerere ambaye ameupongeza sana uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa matokeo haya mazuri ya matumizi sahihi ya fedha za serikali lakini amesisitiza kuendelea kuongeza kasi zaidi katika maeneo ya msingi kama vile ukusanyaji wa mapato kwa kubuni vyanzo vipya na kuongeza kasi zaidi katika vyanzo vilivyopo hasa kwa kuchambua changamoto husika na kuzitatua kwa wakati.
Mhe. Mkuu wa Mkoa huyo aliambatana na waandamizi mbalimbali wa kiserikali kutoka ofisi yake ikiwa ni pamoja na Mlezi wa Mkoa wa Manyara toka OR-TAMISEMI na Ofisi ya mkaguzi Mkazi mkoa wa Manyara. Kwa mujibu wa sheria namba 19 kifungu cha 5 Mkuu wa Mkoa atasimamia shuguli zote za ndani ya mkoa husika kwa maendeleo mapana ya watu wake.
Taarifa ya Mkaguzi ya hesabu kama ilivyowasilishwa na mkaguzi wa hesabu za serikali za mitaa mkoa wa manyara ambapo hoja zilikuwa 43 kati ya hizo 12 zilikuwa hajijafungwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na taratibu za kuzitatua zinaendelea katika hatua mbalimbali. Katika ukaguzi huu ni utaratibu wa serikali wa kawaida katika kujiridhisha kama fedha zilizokusanywa zilitumika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu sahihi, kujiridhisha kama manunuzi husika yalifuata sheria, kanuni na taratibu za manunuzi. Hata hivyo katika miradi ya maendeleo ukaguzi unafanyika kuangalia ubora wa miradi husika kama inaendendana na thamani ya fedha iliyotumika kwa hiyoo siyo kukosoa tu bali ni pamoja na kushauri wapi pa kuboresha ili kuimarisha miradi hii katika uwekezaj kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
Mhe M. Nyerere amewapongeza kwa kupata hati safi kwani ni matokeo mazuri ya utendaji kazi kati ya madiwani na wataalamu wa halmashauri ya wilaya ya mbullu. vigezo vya kupima utendaji kazi wa halmashauri ni pamoja na uwezo wakukusanya mapato ya kutosha ili kuweza kuiendesha ofisi, kupeleka fedha za miradi ya maendeleo 40% na kupeleka 10% ya mikopo kwa vijana wanawake na walemavu na la mwisho ni kujibu hoja kwa nguvu zote.
Katika kikao hicho ililisitizwa kwamba katika mkakati wa kuzitatua hoja hizi ni muhimu wahusika waliosabanbisha hoja kwa uzembe ni lazima hatua zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.