Halmashauri ya Kijiji cha Eshkesh kilichopo katika kata ya Eshkesh Wilayani Mbulu Mkoani Manyara ilipokea ombi la Ardhi yenye ukubwa wa ekari 7000 kutoka kwa kampuni ya Bargweka Farm Ltd.mnamo tarehe 08/04/2010 kwa ajili ya ufugaji ng’ombe wa kisasa aina ya“Boran”
Baada ya ombi hilo kuwasilishwa, halmshauri ya kijiji na mkutano Mkuu wa kijiji cha Eshkesh viliridhia kampuni ya Baragweka ipewe ekari 3903 badala ya ekari 7000 ambazo mwombaji alikubaliana na kijiji atatoa huduma za jamii kama vile maji,mojosho,mashine za kusaga nafaka, zahanati na shule.
Kwa mujibu wa sheria ya Ardhi ya vijiji Na.5 ya mwaka 1999 ombi hilo liliwasilishwa kwa Halmashauri ya Wilaya na hatimaye kwa kamishina wa Ardhi Msaidizi kanda ya kaskazini kwa hatua zaidi za kwa Mhe. Waziri wa Ardhi,Nyumba naMaendeleo ya Makazi. Wakati Waziri akiwa kwenye mchakato mzima wa uhawilishaji alipokea malalamiko kuhusu mchakato mzima wa uhawilishaji wa eneo hili na alisitisha uhawilishaji mpaka maelekezo mengine yatakapotolewa.
Mkurugenzi wa kampuni ya Baragweka Farm Ltd. Alipeleka malalamiko kuhusiana na kusitishwa kwa mchakato wa uhawilishaji wa eneo hilo kwa Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhauri wa Muungano wa Tanzania, ambapo Waziri Mkuu aliunda timu ya wataalam kufuatilia malalamiko hayo mnamo mwezi Mei,2017.
Baada ya timu kupitia malalamiko hayo waliweza kubaini kuwepo kwa mapungufu mengi na Mhe. Waziri Mkuu alitoa maagizo kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara,Kufuatia ziara ya Mkuu wa Mkoa Wilayani Mbulu mwezi februari 2018 . Timu ya Wataalam wa ardhi kutoka ofisini kwake wakishirikiana na wataalam wilayani hapo waliombwa kupitia mchakato huo upya kama iliyoagizwa na Waziri Mkuu. Mchakato uliopitiwa na timu hiyo ulizingatia mapitio ya Mpango wa matumizi bora ya ardhi na kujadili maombi ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa shamba la mifugo katika kijiji cha eshkesh.
Kufuatia kikao cha Baraza maalum la Madiwani lililokaa mnamo tarehe 09/03/2018, baada ya kukaa na kujadili kwa zaidi ya masaa matatu kuhusiana na mchakato uliopitiwa,Madiwani waliohudhuria kwenye kikao hicho maalumu walikuwa madiwani wapatao 23 ambapo waliweza kuhitimisha kwa kuzingatia muongozo na kuhamua kupiga kura, ambapo Madiwani 14 walisema mwekezaji wa kampuni ya Bagweka Farm Limited apewe ekari 988 badala ya ekari 3,903 zilizoombwa.
Aidha Madiwani 6 walisema mwekezaji wa kampuni ya Bagweka Farm Limited apewe ekari 3,903, badala ya ekari 988.
Kikao hicho maalumu cha madiwani kimefanyika kwa agizo la mkuu wa mkoa wa manyara bwana Alexanda Mnyeti ya kutaka kujadali namna ambavyo mwekezaji aliwasilisha malalamiko yake katika ofisi ya Waziri Mkuu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.