Na. Ruth Kyelula
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Joseph Mandoo amewataka maafisa Mifugo wazitumie piki piki walizokabidhiwa kwa ajili ya kusaidia wakulima na watanzania wa Halmashauri yetu ya Wilaya ya Mbulu.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Joseph Mandoo wakati akikabidhi pikipiki saba kwa Maafisa Mifugo wa Halmashauri, mbele ya jengo la utawala, januari 16, 2023.
“Pikipiki hizi tunazikabidhi, mzitunze vizuri. Ni kwa matumizi ya shughuli za serikali, sio za matumizi binafsi. Hasa za utoaji wa huduma za ugani kwenye kata za Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, hasa kata ambazo mmenufaika nazo.Kama Halmashauri tulikuwa na changamoto kubwa.Kwahiyo kazi ya Mkurugenzi ni kutafuta fedha kwa ajili ya kutenga mafuta ili muweze kufanya kazi nzuri kwenye kata mbalimbali.” Alisema Mhe.Mwenyekiti Mandoo.
Aliendelea kusema kuwa, anamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuwahudumia watanzania hasa wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, na akawaasa maafisa ugani wakafanye kazi bora ambazo wananchi watafurahia huduma za ugani kwenye maeneo yenu ya kazi.
Naye Afisa Mifugo wa Halmashauri Nicodemus Michael, alisema kuwa ugawaji wa pikipiki unatoka serikali kuu katika wizara ya mifugo, na sio zoezi la kila mwaka inategemea na serikali ikipata hela kwa ajili ya kuwagawia maafisa mifugo halafu baada ya hapo ikipatikana wanagawa na idadi ya pikipiki inategemea na uhitaji wa eneo husika.
Kwa upande wa Afisa mifugo wa kata ya Tumati, Salumu Lesso, ambaye naye ni mnufaika wa pikipiki hizo alisema kuwa anaishukuru Halmashauri kwa sababu walikuwa wanapata tabu namna ya kuwafikia wafugaji na wakulima ambao wengine ni umbali hata wa km saba (7) kuwafikia. Na kwa sasa tutakuwa na nyenzo ya kuwafikia wananchi na huduma itaboreka tofauti na hapo awali.
Kaimu Mkurugenzi, ndugu Juma Kirimba(Afisa Mazingira)-kushoto akisuhudia tukio lakukabidhi pipikipi
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.