Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mh. Joseph Mandoo Akizungumza Katika Kikao cha Baraza Hilo la Madiwani
Kushoto ni Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt.Chelestino Simbalimile Mofuga Akisamilia Wajumbe wa Baraza la Madiwani
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson S. Kamoga Akizungumza Katika Kikao Hicho
Mh. Mbunge Flatei wa Jimbo la Mbulu, Akisalimia na Kuzungumza na Wajumbe wa Baraza la Madiwani
Wah. Madiwani Katika Muonekano wa Picha Tofauti Tofauti Wakiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani
Wakuu wa Idara na Vitengo Katika Muonekano wa Picha Tofauti Tofauti Wakiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Haya yamejiri katika kikao cha baraza la waheshimiwa madiwani cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2020/2021 kuanzia januari, 2021 hadi machi 2021 kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Gote iliyopo kata ya Dongobeshi, ambapo kubwa ni kuwepo kwa mshikamano wa dhati baina ya wakuu wa idara/vitengo na madiwani kwani bila wataalamu hakuna kitu kitafanyika na bila madiwani hakuna kitu kitapita.
Zaidi imefahamika kwamba ukusanyaji wa mapato hadi machi 2021 ilikua ni kiasi cha milioni mia 9.3 ambayo ni takribani zaidi ya 60% ya makusanyo yote ya mapato kwa mwaka kwa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu vijijini, hata hivyo kuongeza kasi zaidi kwa miezi miwili iliyobaki kwa kusimamia mianya ya utoroshaji wa mapato ili kuweza kufikia lengo zuri na kujipanga kwa mwaka wa fedha ujao wa 2021/2022, kwani usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri utasaidia fedha hizi kukuza wigo wa kuwahudumia wananchi wa halmashauri ya wilaya ya mbulu vijijini.
Kwa sasa changamoto zinazojitokeza ni pamoja na barabara kutokuwa rafiki katika maeneo mengi kiasi kwamba uchukuaji wa mazao katika maeneo ya vijijini ili kwenda kuuzwa mjini umekuwa wa shida na hii imepelekea kuongezeka kwa gharama za usafirishaji na kupunguza faida anayopata mkulima kutokana na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji mazao husika.
Maeneo kadhaa yaliyosisitizwa kuwa 10% ya makundi maalumu yaani vijana, walemavu na wanawake wapewe kipaumbele katika kuwakopesha mikopo yao ili wajikwamue kiuchumi chamsingi ni kuwafuatilia katika marejesho ya mikopo hiyo.
Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt.Chelestino Simbalimile Mofuga katika kuwasalimia wajumbe alisema "ili kuweza kupunguza na kutokomeza mabango ya wananchi pindi viongozi wa juu wanapokuja yasijitokeze ni kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwa kutatua kero zao kwa usahihi na kwa wakati kwa nguvu zote katika maeneo yote kuanzia ngazi ya Kata.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndugu Hudson S. Kamoga ameelezea kwamba ukamilishaji wa bweni la shule ya sekondari ya Yaeda chini litaangaliwa kwa utaratibu mzuri zaidi baada ya kuwasiliana na Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt.Chelestino Simbalimile Mofuga ili tuweze kumaliza bweni hilo kwani taarifa walizozipata awali hadi kupelekea jengo kutokukamilika zilikuwa siyo sahihi. Pia amewahimiza wananchi kujitokeza katika siku za kusikiliza kero za wananchi kwa kila jumanne ya kila juma hapa dongobeshi ambapo anapokea na kero za kata za jirani.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.