kutoka kushoto ni Kiongozi toka DIT,Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, na Kiongozi wa Mzinga wakionesha Hati ya Makabidhiano
Ikiwa ni takribani miaka minne(4) tangu 26/03/2019 - 20/04/2023, ambapo Mkandarasi Mzinga Holding Company kwa kushirikiana na Mhandisi Mshauri kutoka Dar es Salaam Institute of Technology (DIT).
Meza ya Wakandarasi Makamanda toka Mzinga wakiwa wanafuatilia majadiliano wakati wa makabidhiano.
waliopewa dhamana rasmi ya kuanza ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu katika kijiji cha Dongobesh katika eneo la ardhi lenye ukubwa wa ekari 61 linalomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu hatimaye wameweza kamilisha rasmi na kukabidhi jengo hilo.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Joseph Mandoo akiongoza timu ya ukaguzi wa jengo kabla ya Makabidhiano
Mradi huu ulianzishwa kutokana na kugawanyika kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na kuzaliwa Halmashauri ya Mji wa Mbulu ambapo ililazimu Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kuhama Mbulu Mjini na kuhamia hapa Dongobesh ili kutekeleza Sera ya Serikali ya kusogeza huduma karibu na Wananchi.
Viongozi mbalimbali wa timu ya Wahandisi Washauri toka DIT wakifurahi jambo wakati wa makabidhiano
Jengo hili limegalimu kiasi cha Tsh 4 bilioni fedha za ruzuku toka Serikali kuu ikiwa ni ujenzi wa awamu ya kwanza kwa mujibu wa makubaliano ambayo ilikuwa ni Tsh.5.1 bilioni,na ili kukamilisha ujenzi kwa awamu ya pilii tagharimu kiasi cha Tsh 6.3 ili kukamilika.
Muonekano wa Jengo letu la Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Wakikabidhi hati ya matumizi ya jengo kwa uongozi wa halmashauri baada kurizika na ujenzi kwa kiwango kikubwa DIT (Mhandisi Mshauri) ambaye alikuwa msimamizi na mwangalizi wa jengo pamoja na taasisi ya Mzinga aliyekuwa Mkandarasi wamefanya hivyo ili kuruhusu matumizi rasmi ya jengo kuendeleakwa ufasaha nakutoa ruksa kwa halmshauri kuweza kuendelea na taratibu mbalimbali za kiutendaji.
Timu mbalimbali za Wataalam mbalimbali wakiwa katika ukaguzi wa Jengo
Aidha jengo hili litakuwa katika uangalizi wa Mkandarasi kwa kipindi cha mwaka mzima ambapo mkandarasi atakuwa site kwa uangalizi wa jambo lolote litalotokea.
Hiki moja ya Vyumba maalumvilivyofungwa mitambo mbalimbali wataalam wakishuhudia jinsi kinavyofanya kazi.
Wakiongea viongozi kwa nyakati tofauti wametoa rahi kwa watumiaji wa jengo kuwa na uchu wa kile kilichopo kwani itasaidia kutunza na kulinda kuwa ustadi jengo letu ili kusaidia jengo hilo kwa vizazi vijavyo.
Mwenyeki wa Halimashauri pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wakisoma kwa pamoja hati ya Makabidhiano
Jengo hili ni moja ya majengo bora nchini tangu taasisi hii kuanza kujenga,hivyo tunaomba tulinde na kuyatunza ili panapotokea tatizo liweze kufanyiwa marekebisho kwaharaka kwa kipindi hiki cha uangalizi.
Wakandarasi toka Mzinga wakiongozwa na Kamanda Juma(mwenye shati jekundu) wakiendelea toa maelekezo mbalimbali
Kwa upande wa halmashauri umeahidi kuendelea kumtumia DIT kwa shughuli mbalimbali za ubunifu na usanifu kwani bado tunayo mahitaji mengi katika jengo hili.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.