Naibu Waziri wa Elimu wa kwanza kulia alipokuwa akiwasii katika shule ya Sekondari Tumati kukagua Mradi wa ujenzi wa Bweni la Wasichana, anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ndugu Umofuga, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Willaya ya Mbulu ndugu kamoga na Afisa Elimu Sekondari.
William Ole Nasha Naibu Waziri wa Elimu amesema hayo l eo alipofanya ziara ya siku moja Wilayani Mbulu na kukagua baadhi ya miradi ya Elimu kwa kata ya Dongobesh na Tumati.
Akiongea mbele ya Mkutano wa hadhara wamewahimiza wazazi kuwaandiksha wanafunzi kwa wingi kwani kwa sasa elimu ni bure na sio kuwazuia watoto ili waende kuchunga, akitoa mfano Kutoka jimboni kwake loliondo amesema kwa hivi sasa wanaochunga ni Wazee na sio watoto.
Naibu Waziri wa Elimu akipata maelekezo kwa Kina juu ya ujenzi wa Bweni la wasichana toka kwa Mhandisi wa Ujenzi ndugu Bundala
Aidha amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili kujikwamua kielimu na kuja kuwasaidia wazazi kwa maendeloe ya baadae na kuwaagiza viongozi kuanzia ngazi za vijiji hadi juu kwa wanafunzi wanaomaliza darasa la saba hawaondoki maeneo yao kwenda kufanya kazi za ndani wakati wakiwa wanasubiri matokeo yao yakuhitimu darasa la saba kwani wengi wao wanapondoka kuna wanyima fursa ya kuendelea na masomo.
Naibu waziri ole nasha akiongea na wanafunzi wa Shule binafsi ya Wasichana Gote iliyoko kata ya dongobesh.
Naibu Waziri huyo ameendelea kuwaomba viongozi kuwa mfano wa kuigwa katika jamii pale wanapopata dhamana ya kusimamia fedha za Serikali katika miradi iliyokusudiwa.
Mhe. Flatei G.Massay akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tumati hii leo katika Ziara ya Naibu Waziri wa Elimu Mhe. William Ole Nasha
Mhe. William Ole Nasha akiwa amavaa vazi la Asili ya Kiiraqw hii alipofanya ziara yake katika kata ya Tumati na Dongobesh.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mwenye T.shirt nyeusi aliyekaa akiwa na baadhi ya Viongozi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Waziri wa Elimu hii leo katika ziara ya siku moja wilaya humo.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.