Na Ruth Kyelula, Mbulu DC
Maafisa Habari Serikalini wameagizwa kutangaza miradi na shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ili wananchi wajue ikiwemo kujibu hoja za uongo zinazotolewa na watu dhidi ya serikali.
Akifungua mkutano wa siku tatu wa chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Uliofanyika AICC Arusha, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro, kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko, amesema maofisa hao wanawajibu mkubwa wa kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ili watu waone ukubwa wa kazi zinazofanywa na serikali katika nchi hii. Aliyasema hayo Februari 27,2024.
Mgeni rasmi Dk. Damas Ndumbaro wa kwanza kushoto akiwa kwenye meza kuu na wageni waalikkwa kwenye kikao kazi cha Maafisa Habari AICC jijini Arusha.
“Baadhi ya watu hawaoni ukubwa wa karatasi nyeupe ulivyo sasa ni wajibu wenu kueleza kazi zinazofanywa na serikali ikiwemo kujibu hoja za uongo dhidi ya serikali, lazima mjue kujibu fitna na zengwe”. Alisema Dk. Ndumbaro.
Alisisitiza kuwa hata serikali inapigwa fitna, sasa ni kazi ya maafisa habari kujibu fitna na zengwe kwani hivi sasa zama za teknolojia ya habari imekua na ni nzuri ila inachangamoto zake kupitia mitandao ya kijamii.
Alisema moja kati ya changamoto kubwa iliyoletwa na mitandao ya kijamii haijui ni nani mtoa habari na nani anayepaswa kujua hii ni habari hivyo zitumiwe changamoto hizi kwa ajili ya kujibu hoja na lazima mafunzo ya mara kwa mara yatolewe ya matumizi ya mitandao ya kijamii.
Baadhi ya Maafisa Habari wa Halmashauri akiwemo Afisa habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Ruth Kyelula wa tano kulia walio simama, wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo na Msemaji mkuu wa serikali Bw. Mobhare Matinyi alisema Maafisa Habari na Mawasiliano wa serikali nchini wametakiwa kuzungumzia mafanikio makubwa yanayofanywa na serikali katika sekta zote nchini.
Msemaji Mkuu wa Serikali Mabhore Matinyi akizungumza na Maafisa Habari katika ukumbi wa AICC jijini Arusha
Matinyi alisema kazi kubwa imefanyika hapa nchini katika sekta na maeneo mbalimbali, hivyo anatarajia maafisa habari hao kuzungumzia kila sekta bila kujali amebobea eneo gani.
“Fani hii ni pana sana, natarajia kila afisa habari na mawasiliano aweze kuzungumzia kila sekta au eneo katika uchumi, jiografia, mazingira na maeneo mengineyo hata kama umebobea eneo jingine au umehamia eneo jipya.” Alisema Matinyi.
Mgeni rasmi Dk. Damas Ndumbaro akizindua jarida la TAGCO katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Aidha Matinyi amesema kwamba maafisa habari hao wanao wajibu wa kutekeleza yale yanayofanywa na Taasisi zao kwa kupata mrejesho toka kwa wananchi pamoja na kuhakikisha wanasaidia kukuza taswira nzuri za taasisi hizo.
Kwa upande mwingine Msemaji Mkuu huyo amewakumbusha maafisa habari hao kuhakikisha wanatuma ripoti zao za kila mwezi Idara ya habari – maelezo ambao wana jukumu la kusimamia na kuratibu shughuli za kiserikali.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.