Komredi Heri James Mkuu wa Wilaya ya Mbulu (Mgeni rasmi) akipokea stuli toka kwa Meneja wa kanda wa Benki ya Nmb ndugu Dismas Prosper.
Madawati pamoja Stuli zilizodhaminiwa na Benki ya NMB
Akipokea leo msaada uliotolewa na Benki ya Nmb Mbulu, Mgeni rasmi Komredi Heri James Mkuu wa Wilaya amesema kuwa anawashukuru Nmb kwa kuwaona na kuweza kuwasaidia vifaa hivyo licha ya wahitaji kuwa ni wengi, msaada leo mnao utoa leo sio kidogo kabisa kama inavyotamkwa. Anapenda kuipongeza nmb kwa kuwa mstari wa mbele kwa kuunga juhudi za dhati za Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wetu katika sekta ya elimu na afya.
Meneja Mahusiano na Biashara wa Kanda wa Benki ya NMB Bi. Chiristabel Hiza akisalimiana na Mgeni rasmi
Meneja wa Kanda wa Benki ya NMB ndugu Dismas Prosper akisalimiana na mgeni rasmi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu ndugu Fred Myenzi akisalimiana mgeni rasmi Komredi Heri Jame Mkuu wa Wilaya ya Mbulu.
Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mhe. Flatei Massay akisalimiana na mgeni rasmi Komredi Heri James Mkuu wa Wilaya ya Mbulu.
Ili kuonesha dhamira njema waliyonayo wadau wetu amewaomba wanafunzi,walimu na wananchi kuvitunza vifaa vyetu kwa bidii sana ili visaidie kwa leo na kesho.
Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Bi. Sarah, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbulu Mhe.Joesph Mandoo wakiteta jambo la Viongozi wa Benki
Bi. Sarah Katibu Tawala akiongea jambo wakati wa hafla ya makabidhiano
Komredi James pia ametoa wito kwa wadau wengine mbalimbali kuiga mfano unaotolewa na wenzao kwani wana wajibu wa kurudisha shukurani kwa wananchi kwa kugawana faida wanayokuwa wanakusanya ilikuunga juhudi za dhati za maendeleo, kwani mafanikio hayaji bila kuungana.
Meneja wa Benki ya NMB Wilaya ya Mbulu ndugu Rogate Iranga akiongea jambo.
Meneja wa Beki ya NMB Mbulu akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halamashauri ya Wilaya ya Mbulu
Aidha napenda kumpongeza Mhe. Flatei Mbunge wa jimbo la Mbulu kwa kuwa ni mmoja ya wabunge anawaohitaji kwani amekuwa mstari wa mbele katika maendeleo hii.
Meneja wa Beki ya NMB Mbulu akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halamashauri ya Wilaya ya Mbulu.
“Ikiwa katika kuendana na Kauli mbiu inayosema Nmb karibu yako,benki yetu leo tumeamua kuja karibu yako kwa kuungana nanyi katika kusukuma maendeleo kwa wananchi kwa kugusa kada mbalimbali za elimu na Afya .
Tumeamua kuja kusaidiana na kutoa shukrani kwa wananchi ikiwa nikurudisha sehemu ya faida kwa wananchi wa Mbulu hasa kwa kugusa kada ya elimu,kwani benki yetu imekuwa na utamaduni wa kutoa sehemu ya kile tunachokikusanya na kukipata”. hayo yamesemwa leo na Meneja wa Benki Nmb wa Kanda ndugu Dismas Prosper wakati akikabidhi vifaa hivyo kwa mgeni rasmi.
Wananchi waliojitekeza katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Bishop Hhando.
Mbunge wa jimbo la Mbulu Mhe. Flatei Massay akichangia mada hata hivyo aliweza kutoa msaada wa chakula wa wananfunzi wa Sekondari ya Bishop Hhando gunia 30 za mahindi
Msaada huu tunaouto ni kwa ajili ya shule tano za Sekondari ya Bishop Hhando, Tlawi, Maghanga, Gunyonda na shule ya Msingi Magong.
Aidha vifaa tunavyotoa leo ni Meza 50 na Viti 50 vyenye thamani ya shilingi Milioni tano kwa shule ya Sekondari Bishop Hhando,Meza 50 na Viti 50 shule ya sekondari Maghang venye thamani ya shilingi Milioni tano, meza 50 na viti 50 kwa shule ya msingi Magong yenye thamani ya shilingi Milioni tano, Meza 100 na Viti 100 kwa ajili ya Sekondariya Tlawi vyenye thamani ya shilingi Milioni Sita pia Stuli 100 za Sekondari Gunyoda vyenye thamani ya shs. Milioni tatu.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Bishop Hhando wakiwa katika picha ya pamoja
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki wakiwa katika picha wakati wa makabidhiano.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.