Kutoka kulia ni Mweka hazina wa Halmashauri bwana Kagaruki akiwa na Afisa Mipango wa Halamshauri bwana Kundy wakifuatilia kikao cha Baraza la Madiwani
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imepokea kiasi cha Tsh. billion 2,346,489 553.60 kwa ajili ya Miradi ya maendeleo kwa ajili ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa shule za msingi na sekondarina miradi mbalimbali.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.
Kutoka Kulia ni Mhe. Ester Joel Diwani Viti Maalumu Dongobesh na mweyekeiti wa kamati ya Uchumi akiwa na Mhe. Nada Diwani masieda na Mwenyekiti kamati ya Elimu, Afya na Maji
Hayo yamethibitishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mhe.Joseph G. Mandoo katika kikao cha robo ya tatu cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi uliawa halmashauri chenye lengo la kujenga na kutatua changamoto mbalimbali ndani ya Wilaya ya Mbulu.
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Mhe. Joseph Mandoo( Dwani kata yDinamu) akifuatilia mjadala wa kikao cha Baraza
Miradi hiyo imepelekwa katika Vijiji vyote Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambapo kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Gregory Massay anasema hana budi kupeleka salamu za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe.Dokta Samia Hassan Sullu kwa kuipa halmashauri fedha za kutosha za maendeleo na hata kusema kuwa bado kuna fedha nyingi zinaendelea kuja.
Mhe. Flatei Massay Mbunge akichangia Mada katika kikao cha Baraza
“Usipokuwa na Moyo wakushukuru kidogo hata kile ulichopewa kidogo huwezi ridhika” alisema hayo mhe.mbunge
Wataalamu wa Halamshauri wakifuatilia mijadala mbalimbali ya kikao cha Baraza kutoka Kulia Afisa Utumishi bi Neema, Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Praxeda,Mwanasheria wa Halmashauri Wakili kaijage na Afisa Elumu Msingi Bi Fatu Msangi
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mbulu wakiwa katika Kikao cha Baraza
Kwa upande wa Madiwani walioweza kuchangia michango mbalimbali ya iliyowasilishwa na kamati za kudumu wameendelea kuwapongeza wataaalam na kuwaomba kusimamia ipasavyo na kwa bidii fedha zinazoletwa ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Mhe.Joseph Diwani Kata ya Dongobesh akifurahi kusikia dongobesh anaenda kuletewa maendeleo zaidi wakati wa kikao cha baraza
Makamu Mwenyekiti na Diwani kata ya Bashay akichangia mada wakati wa kikao cha Baraza
Mhe. Elimina Shishi Diwani Viti Maalum akisoma kwa umakini kablasha linalowasilishwa.
Aidha akiongea kwa niaba ya Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kaimu Mkurugenzi ndugu Moses Nduligu ameendelea kuwahakikishia wajumbe wa baraza hilo kuwa wamejipanga katika kutekeleza, kusimamia na kulinda kwa ufasaha miradi inayoletwa na inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ndani ya halmashauri. Hivyo nitoe lai kwa waheshimiwa kuwasisitiza wananchi kutoa ushirikiano pale mradi unapokuja ndani ya kijiji.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu akichangia mada wakati wa Kikao cha Baraza
Kwa pamoja tunaijenga Mbulu yetu kwa kuwatumikia wananchi, alihitimisha kwasema hayo kaimu Mkurugenzi.
Mhe. Bajuta Diwani wa kata ya Yaeda chini akiwa anasoama kablsha linalowasilishwa katika kikao cha Baraza.
waendesha kikao cha Baraza(CC)wakiendeleana kikao cha Baraza
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.