Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mheshimiwa Komredi Queen Sendiga, amefanya ziara maalumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na kuzungumza na Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wataalam katika kikao cha Babaraza maalumu ya kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za mwaka2022
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Sendiga ameipongeza Halmashauri kwa kuendelea kupata hati safi kwa mara tatu mfululizo na kama kungekuwa na tuzo ya ushindi toka Serikalini basi wanastahili kuipata, aidha amewapongeza kwa kazi kubwa na nzuri ya kukusanya Mapato, kusimamia miradi na kusimamia huduma kwa wananchi.
Komredi Queen ameitaka Halmashauri kuweka mkakati maalumu wa kujibu na hatimae kumaliza hoja zote zilizo ibuliwa katika Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Pamoja na mambo mengine Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amesisitiza umuhimu wa kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya Ukatili wa kijinsia katika jamii, kwa kuwataka Viongozi na Wananchi kuwabaini na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wahusika wote wanaohusika na vitendo hivyo viovu katika jamii.
#Kwapamoja,Tunaijenga Mbulu yetu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.