Aliyesimama ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Wilaya ya Mbulu, Mhe. Sezaria. V. Makota ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Abubakar. A. Kuuli Wakiwa Katika Kikao Kazi Hicho Kilichofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Dongobesh Tarehe 19.08.2022
Aliyesimama ni Mhe. Sezaria. V. Makota Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Anayefuatia Kushoto ni Mhe. Mbunge Flatei G. Massay wa Jimbo la Mbulu Vijijini na wa Mwisho ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mhe. Joseph G. Mandoo, Wakiwa Katika Kikao Kazi Hicho.
Pakua kadhaa za kikao hicho hapo chini
~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~
Haya yamejiri leo ambapo Mhe. Sezaria Makota Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ambaye katika kikao kazi hiki ni Mwenyekiti wa sensa kwa Wilaya ya Mbulu, kikao hiki kimefanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Dongobesh Kata ya Dongobesh Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu. Wahusika wa mafunzo haya ni Kamati ya sensa ya wilaya, waheshimiwa madiani, wenyeviti wa vijiji, wawakilishi wa dini, wawakilishi wa kundi maalumu la walemavu na wazee maarufu.
Mhe. Sezaria V. Makota amesema lengo kuu la kikao kazi hiki ni uhamasishaji wa sensa katika maeneo yetu kwasababu sisi ndiyo timu ya ushindi kwa wilaya hivyo tunatarajia mtusaidie kuhamasisha jamii yote huko ili kuhakikisha zoezi zima la sensa linafanikiwa katika wilaya ya mbulu ambapo takwimu za watu, mifugo, majengo na vingine vinatakiwa vihesabiwe kwa maslahi mapana ya mwananchi mwenyewe, Halmashauri ya Mbulu na Taifa kwa ujumla.
Mhe Sezaria aliendlea kusisitiza kwamba wakati mtakapokuwa mnawatembeza makarani basi ni muhimu msiruke nyumba hata moja na pia wahusika wahamasiheni kutoa taarifa sahihi ili kuweza kupata uhalisia wa takwimu hizi zitakazowezesha serikali kufanya maamuzi sahihi ya eneo letu katika kuongeza nguvu ya kutoa huduma mbalimbali hususani katika afya yaani zahanati, na vituo vya afya, katika elimu ni shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na vya elimu ya juu, miundombinu ya huduma za umeme, maji na marabara kwa pamoja vyote hivi havipangwi tu bila kujua idadi ya watu na shughuli zao.
Kuna vijiji ambavyo vina makabila yenye mahitaji maalumu ambavyo ni vinne Yaeda chini, Endanyawish, Mongo wa mono na Domanga ambavyo wanaishi jamii ya wahadzabe wananchi wa maeneo haya kutakuwa na kitoweo cha wanyama pori.
Hata hivyo imefahamika kwamba makarani watarudi zaidi ya mara moja katika kaya moja kwa kuwa kutakuwa na madodoso tofauti na kwa siku tofauti lakini siku ya sensa husika ni tarehe 23.08.2022 ambapo amewaomba wananchi kuwepo nyumbani au wakiondoka basi awepo mtu ambaye atatoa taarifa sahihi ya kaya husika na nyaraka muhimu kama vile vitambulisho vya NIDA na vitu vingine muhimu.
Katika mafunzo haya ya uhamasishaji viongozi hawa walikumbushwa kwamba sensa ndiyo kitovu kikuu cha kupanga maendeleo na mtu atakayehesabiwa ni yeyote aliyelala ndani ya nchi yetu haijalishi ni tanzania au simtanzania usiku wa kuamkia siku ya sensa jumanne ya tarehe 23.08.2022. Imefahamika kwamba kutakuwa na makarani 691 ambao wameshafundishwa vizuri kabisa katika vituo 3 yaani Kituo cha elimu cha Gote, Kituo cha shule ya sekondari Dongobesh na kituo cha Haydom katika shue ya seokondari ya Dr. Olsen.
Katika mafunzo yaliyokuwa yakifanyika kwa makarani, maafisa tehama na watu wa maudhui kulifanyika pia zaozi la kujifunza kwa vitendo eneo la kazi (site) ambapo kwa halmashauri ya wilaya ya mbulu walitumia kata ya Dongobesh na kata ya Bashay kwa majaribio na sio zoezi halisi la sensa ila ilikuwa ni kwa ajili ya kuwapima na kuwaongezea uwezo wa kujua mazingira yatakavyokuwa katika sehemu zao za kazi imefahamika, hivyo zoezi halisi bado.Katika kuhakikisha kila mtu anahesabiwa uelimishaji na ushawishi ndiyo unaopewa kipaumbele lakini kwa wanaokataa au kuleta vurugu katika zoezi hili atashugulikiwa kwa mujibu wa sheria ya takwimu sura ya 351. Siku ya sensa ni moja tarehe 23.08.2022 lakini kuna taarifa mbalimbali za madodoso wataanza tarehe 21-22.08.2022 kwa dodoso la jamii, dodoso kuu tarehe 23-28.08.2022 na dodoso la majengo kuanzia kuanzia tarehe 29-02.08.2022
Katika hitimisho viongozi wote kwa ujumla wao, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Abubakar A. Kuuli, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mhe. Joseph G. Mandoo, Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe.Flatei Massay na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Sezaria V. Makota wanamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia S.H. kwa kutoa fedha za kugharamia jambo hili muhimu la sensa lakini pia kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi mikubwa mbalimbali kwa wananchi wa Mbulu kwa kama vile Barabara ya lami Karatu mbulu Haydom Singida yenye gharama zaidi ya bilioni 500, vituo vya afya, shule za msingi na sekondari maji na barabara za hapa makao makuu ya halmashauri ya Mbulu Dongobesh tunamshukuru sana MUNGU ampe maisha marefu.
Sensa kwa maendeleo, jiandae kuhesabiwa.
Sensa hoyeeeeeeeeeeee.......
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.