Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imesema hadi Februari 2024, Sh. bilioni 13.5 zimetolewa kwa ajili ya kulipa posho za madiwani katika halmashauri 168.
Vilevile, Sh. bilioni 1.15 zimetolewa kwa ajili ya kulipa posho za wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa.
Naibu Waziri katika ofisi hiyo, Dk.Festo Dugange alibainisha hayo jana bungeni jijini hapa alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Mbulu Vijijini (CCM), Flatei Massay.
Mbunge huyo alihoji lini serikali itawalipa posho wenyeviti wa vitongoji na vijiji na kuongeza posho ya madiwani ili kuwasaidia kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Akijibu swali hilo, Dk.Dugange alisema serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.
“Serikali imeendelea kulipa posho za wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo,”alisema.
Naibu Waziri alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/24, serikaliimetenga Sh. bilioni 1.7; hadi kufikia Februari, mwaka huu, Sh. bilioni 1.15 zilikuwa zimetolewa kwa ajili ya kulipa posho za wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.