Wafanyabiashara Maarufu, Mzee Joshua Giyee na Gabriel Gurti wa Dongobesh Wakiwa Katika Ghala la Mazao la Maretadu Kwa Zoezi la Ufunguaji wa Ghala Hilo Kata ya Maretadu.
Muonekano wa Picha ya Mbele ya Ghala la Mazao Kata ya Maretadu.
Muonekano wa Picha ya Nyuma ya Ghala la Mazao Kata ya Maretadu.
Wafanyabiashara Maarufu, Mzee Joshua Giyee na Gabriel Gurti wa Dongobesh.
Kutoka Kushoto ni Mh.Diwani Z. Maega wa Kata ya Maretadu, Mh.Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar Abdallah Kuuli na wa Mwisho ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Maretadu.
Aliyeshika Biblia ni Padri James wa Parokia ya Bashay - Wilaya ya Mbulu Akisoma Neono wakati wa Ufunguzi wa Ghafla Hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar Abdallah Kuuli Akizungumza Katika Mkutano Huo.
Katika Hafla Hiyo Padri James, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar Abdallah Kuuli, Mh.Mbunge Flatei Massay na Wafanya Biashara Wawili Dongobeshi Mzee Joshua Giyee na Mzee Gabriel Gurti Walivishwa Mavazi Rasmi ya Kimila Kama Ishara ya Ushujaa na Upendo wa Dhati kwa Wananchi wa Kata ya Maretadu.
Maombi na Sala Kutoka kwa Viongozi wa Dini Wakiongozwa na Padri James Katika Halfa Hiyo.
Mh.Mbunge Flatei Massay Akizungumza Katika Mkutano Huo.
~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~
Katika hafla hiyo iliyojawa na furaha kubwa iliyohudhuriwa na viongozi wa dini kama vile Padri James wa Parokia ya Bashay, wazee maarufu, Mh.Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar Abdallah Kuuli na wengine wengi.
Furaha, shangwe, Hoihoi, nderemo na vifijo vilitawala katika viwanja vya ghala kuu la Kata ya Maretadu wakati na baada ya makabidhianao hayo. Ghala hili ni la Ushirika wa Kata ya Maretadu ambapo shuguli nyingi za kiuchumi na kijamii zilikuwa zikifanyika katika ghala hili ikiwemo uhifadhi wa mazao na pembejeo za wananchi kwa bei nafuu, kituo cha kununua na kuuza bidhaa mbalimbali za wananchi hayo ndiyo yalikuwa malengo ya msingi ya kuwepo kwa ghala hili.
Lakini mwaka 2008 ghala hili lilifungwa kutokana na kutii amri ya Mahakama kufanya hivyo ili kuhakikisha Kata ya Maretadu wanalipa gharama za kampuni ya Mzee Joshua Giyee na Gabriel Gurti wa Kata ya Dongobesh zilizotokana na kufanya kazi ya ukandarasi katika Sekondari ya Kata ya Maretadu wa kuleta malighafi za ujenzi yaani kokoto, mchanga na mawe kwa kiasi kisichopungua Tsh.11 milioni.
Hata hivyo wazee hawa wawili na wananchi wa Kata ya Maretatdu kwa ushirikinao wa Mh.Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu walikaa na kuona na ni vema hili jambo likaisha kwa maridhiano ili wananchi waondoke na kikwazo cha kudidimia kwa maendeleo ya shuguli za uchumi ni kijamii kwa kata nzima ya Maretadu jambo lililofanikiwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.
Katika hali isiyo ya kawaida viongozi wa dini waliomba sana ili kuepusha laana katika ardhi na wananchi wote na kushukuru kwa wazee hawa kutodai fidia ya gharama za uendeshaji wa kesi ya kiasi cha zaidi ya Tsh. 100 milioni jambo lililopongezwa sana na wananchi hawa.
Katika hafla hiyo Padri James, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw.Abubakar Abdallah Kuuli, Mh.Mbunge Flatei Massay na wazee hawa wawili wa Dongobeshi Joshua Giyee na Gabriel Gurti walivishwa mavazi rasmi ya kimila kama ishara ya ushujaa na upendo wa dhati kwa wananchi wa Kata ya Maretadu.
Kwa wakati tofauti Mh.Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay ni kiongozi wa mfano mzuri wa kuigwa kwani anashirikiana vizuri kabisa na wananchi na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu katika kutatua kero mbalimbali za Jimbo lake la Mbulu haya ni maneno ya ujumla kutoka kwa wananchi wa kata ya Maretadu na viunga vyake.
Kupitia halfa hii Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw.A.A.Kuuli amewaagiza Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha kila mradi unapoanzishwa ushirikishe wananchi wa eneo husika kwani ndyo wadau wakuu wa mradi wao ndiyo wataamua kupitia serikali zao za vijiji, vikao vya kamati za maendeleo za kata na mikutano mikuu ya wananchi hii itapelekea kutokuwa na migogoro isiyokuwa ya lazima. Mkurugenzi huyo alisisitiza kwamba "wananchi msisite kutoa taarifa kwa jambo lolote ambalo mnaona haliendi vizuri kwa muda ule ule jambo linatokea ili ofisi yake iweze kuchukua hatua mapema kwan itasaidia kupunguza kero katika jamii".
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.