Na, Ruth Kyelula, Mbulu DC
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Joseph Mandoo, alisema kuwa Mpango wa mapendekezo ya bajeti ya matengenezo ya barabara TARURA lazima ulenge mahitaji ambayo yanawawezesha wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa ujumla kuweza kupata mawasiliano.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu wakiwa kwenye kikao cha bajeti cha TARURA
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Joseph Mandoo, wakati akifungua kikao cha baraza la Madiwani cha mapendekezo ya bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2024/2025 katika ukumbi wa halmashauri Machi 07, 2024.
Naye Mbunge wa Mbulu vijijjini Mheshimiwa Flatei Massay alisema kuwa anamshukuru Mhe. Raisi kwa kuwapatia fedha kwenye sekta ya maji kwenye wilaya ya Mbulu tumepata bilioni arobaini na nne (44) kwa mwaka wa fedha unaoendelea , na alisema bajeti kama hii haikuwahi kutokea kwa Mbulu vijijjini.
Mbunge Flatei Massay akichangia hoja kwenye Baraza
Kaimu Mkuuu wa Wilaya ya Mbulu, Geofrey Nyumainzu, kwa niaba ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya amewapongeza ofisi ya TARURA wilaya ya Mbulu, kwa kazi kubwa na nzuri ambayo wanaendelea kuifanya.
“Wote ni mashahidi tumeona mvua ambavyo zimeharibu miundombinu ya barabara, lakini wamekuwa wakijitahidi ambavyo kuna uwezekano wa kuweza kufanya yale marekebisho ya muda ili kuweza kupitika basi wameweza kufanya hivyo, kwa hiyo niwapongeze sana kwa kazi kubwa mnayoifanya”. Alisema Nyumainzu.
Baadhi ya wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu walioshiriki kikao cha Baraza la bajeti cha TARURA
Lakini pia aliwashukuru waheshimiwa Madiwani kwa namna ambavyo wameendelea kutoa ushirikiano kwa ofisi zote za serikali kwa kuwa kila wanapoona kuna jambo linatakiwa lifanyiwe kazi wamekuwa wakisema na wao Wilaya kama watekelezaji wamekuwa wakichukua hatua na mambo yanaenda.
Kwa upande wa Meneja wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) Wilaya ya Mbulu, Mhandisi Nuru Hondo alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/25 wamependekeza kiasi cha shilingi 3,512,690,000.00 kwa ajili ya kazi za matengenezo, maendeleo, usimamizi wa kazi za barabara na utawala.
Meneja wa TARURA Wilaya ya Mbulu, Mhandisi Nuru Hondo, akisoma taarifa ya bajeti yao ya fedha ya mwaka 2024/25
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.