Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti (mwenye shati la bluu bahari) Akienda Kukagua Kaya za Wanufaika na Mpango wa TASAF Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Kata ya Bashay Kijiji cha Bashay.
Wa Pili Kutoka Kushoto ni Ndugu Emmanuel John Buhhay ni Mnufaika na Mpango wa Kuhudumia Kaya maskini katika
Mpango wa TASAF Kijiji cha Bashay Kata ya Bashay
Wa Kwanza Kutoka Kushoto (T-shirt nyekundu) ni ndugu Philipo John Buhhay ni Mnufaika na
Mpango wa Kuhudumia Kaya maskini katika Mpango wa TASAF Kijiji cha Bashay Kata ya Bashay
Miradi Waliyoiibua na kuitekeleza Kama Inavyoonekana Hapo Juu
Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt.Chelestino Simbalimile Mofuga Akimkaribisha Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti Akisalimia Wananchi Kata ya Dongobeshi Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Hayo yamejiri katika ukaguzi wa kaya maskini zinahudumiwa na serikali kupitia mpango wa TASAF ambapo Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti alitembelea kaya kadhaa zikiwemo mbili za Kijiji cha Bashay Kata ya Bashay kwa ndugu Emmanuel John Buhhay na ndugu Philipo John Buhhay wote wa eneo hilo hilo.
Katika ukaguzi huu ilionekana kwamba hawa wanuafaika kwa mwaka 2015 kabla hawajaingia katika mpango wa TASAF walikuwa katika hali ngumu sana ya kujikwamua kiuchumi katika familia zao lakini bada ya kujiunga na mpango huu kupitia kuchaguliwa katika mikutano mikuu ya kijiji sasa hivi kila mtu anambuzi zaidi ya 6, nyumba ya kwake ya kuishi tofauti na mwanzo wote walikuwa wanaishi nyumba za kupanga.
Mbali na hii miradi pia wana mashamba ya mazao mbalimbali ikiwemo mahindi. Hivyo wanaishukuu sana serikali kwa kuwasaidia.
Hata hivyo Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti alipitia kata ya Dongobeshi kuwasalimia wananchi kabla ya kuelekea Wilaya ya HananG huku akisisitiza wananchi kujiunga na mfuko wa bima
ya afya iliyoboreshwa kwa manufaa ya familia zao kwani ni Tsh. 30,000/= ili uweze kupata matibabu mwaka mzima.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.