Shirika la Uratibu na Ushirikiano la Utruruki (TIKA) ambalo linahudumu kama Wakala rasmi wa msaada wa Kiufundi wa Jamhuri ya Uturuki limeahidi kujenga Kituo cha Utamaduni ili kutunza Utamaduni wa Mhazabhe anayeishi Mstuni.
Hayo yamebainishwa na wawakilishi wa TIKA toka Uturuki walipofanya ziara ya siku moja katika bonde la Yaeda chini, wakiwa katika ziara hiyo waliyoambatana na Mwenyeji wao Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Veronica waliweza kutembelea maeneo wanayoishi wahazabhe na kufurahishwa na kukutana na jamii hii licha yakuwa wanaishi kwa kula matunda na mizizi ya porini na kutoa nafasi ya kusikiliza changamoto zinazowakabili ili waweze kupatiwa misaada kadiri shirika litakavyoweza.
Akiongea kwa niaba ya Wahzabhe ndugu Athuman alibainisha kuwa kutokana na jamii yao kuishi porini wanayo sababu kubwa yakuendeleza Utamaduni na kulinda Mila zao, aidha ndugu Athumani aliendelea kusema kwa wasasa wanahitaji kupatiwa Msaada wa kujengewa kituo cha Utalii ambacho kitawasaidia kulinda na kutunza Utamaduni wao na hata kusaidia kupata kipato kwa ajili ya mahitaji mbalimbali.
Alienda kusema pia wanahitaji kujengewa shule kwani Watoto wao wanatumia umbali mrefu Zaidi ya Km kumi (10) kufikia shule ya Jirani,Athuman alisema kwa sasa wameanzisha shule ya Awali licha kuwa ni ya miti toka eneo la makazi yao ambapo wametenga ekari 40 kwa ajili ya ujenzi.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.