Na Ruth Kyelula, Mbulu DC,
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu, Paulo Bura ambaye amemwakilisha mkuu wa Wilaya ya Mbulu Veronica Kessy, amewataka watendaji wa vijiji, wenyeviti wa vijiji na watendaji wengine wa kata waweze kuwapa ushirikiano wa kila hali shirika la UCRT ili kile walichokuja nacho kiweze kuwanufaisha wananchi wa wilaya ya Mbulu na lengo lao la makusudi na nia yao njema iweze kutimia.
Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Mbulu, Paulo Bura, wakati akifungua kikao cha uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa Mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji sita, chini ya Ujamaa Community Resource Team (UCRT), uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Machi 19, 2024.
Picha ya pamoja ya meza kuu na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu wakati wa uzinduzi wa mradi wa UCRT.
“Lakini sisi tulioingia kwenye awamu hii vijiji hivi sita, pia tujue sisi ni mfano wa vijiji vingine ambavyo vimeendelea kuombwa ili viingie kwenye mradi,wale wa awamu ya kwanza vijiji vitano hawajatuangusha,ndio maana maombi yalivyorudishwa kwa wahisani wa maendeleo wakaona vile vijiji vilifanya vizuri, kwahiyo hata hivi vijiji sita vikifanya vizuri vinaweza kuwa fursa na mlango kwa ajili ya vijiji vingine, kwa hiyo sisi ambao tuliopata fursa na bahati hiyo tuweze kuitumia vizuri ili basi tuweze kufungua milango kwa vijiji vingine kuweza kunufaika na mradi huu mzuri kwa ajili ya hifadhi ya mazingira lakini pia kwa ajili ya uchumi wa wananchi wetu.” Alisema Bura.
Viongozi wa vijiji na kata ambao ni wanufaika wa mradi.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa Hamashauri ya wilaya ya Mbulu Petro Tarmo aliwaomba wale wanufaika wa mradi wa zamani waendelee kutoa ushirikiano na hawa wapya waendelee pia kutoa ushirikiano kwa UCRT, waendelee kutoa elimu kwa wananchi na kuepuka migogoro ya mipaka ambayo inaweza kupelekea changamoto kwenye mradi. Waepukane na migogoro ili waende kwenye maslahi mapana ya wananchi. Aidha mratibu wa Ujamaa Community Resource Team (UCRT), Dismas Meitaya ameushukuru uongozi wa wilaya Mbulu kwa ujumla kwa kuweza kuushirikiana nao vizuri kwa Zaidi ya miaka ishirini waliyokuwa wakitekeleza miradi yao. Ikiwemo ofisi ya mkuu wa Wilaya, ofisi ya Mkurugenzi, wataalam wa hamashauri na viongozi wa vijiji.
Viongozi wa vijiji na kata ambao ni wanufaika wa mradi.
Alisema kuwa malengo makuu ya UCRT ni kuwezesha jamii ya asili kuweza kumiliki, kusimamia na kunufaika na ardhi. Na wamelenga Zaidi kwenye jamii ya wakusanya matunda, ambao ni wa hadzabe na waakie, wamaasai, wadatoga pamoja na wafugaji – wakulima wabatemi na wa iraqw.
Watuumishi wa Halmashauri wakifuatilia kwa umakini ufunguzi wa mradi wa awamu ya pili wa UCRT.
“Huu mpango ni shirikishi sana, wakina mama wanapewa kipaumbele na washiriki kisawa sawa. Kwa hiyo nataka kuona jamii ya akina mama na vikundi vingine wakiwa mstari wa mbele kushirikishwa kwa kila hatua ambayo tunakuja kufanya.” Alisema Dismas.
Alibainisha vijiji lengwa sita vya mradi katika bonde la Yaeda na ziwa Eyasi ni Garbabi, Yaedakati, Dirim, Endalat, Murkuchida na Endamilay.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.