Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu leo tarehe 16/03/2019 imewekeana saini kuanza rasmi ujenzi wa jingo la Utawala litakalo jengwa katika mji wa Dongobesh chini ya kampuni ya “Mzinga Holding Company”
Akiongoza zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ndugu Christino Mufoga amewataka kampuni hiyo kuanza ujenzi huo haraka iwezekanavyo ili kuenda na wakati,Ujenzi huo wa jengo unatagemewa kukamilika kwa mwaka fedha 2019/2020.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mhe. Joseph Mandoo akisaini vitabu vya Mikataba baina ya kampuni ya Mzinga
Ujenzi unategemwa kugharimu kiasi cha billioni 6,356,510,317 ambapo utajengwa kwa awamu mbili,katika kiasi hicho cha fedha zinazotarajiwa tumika kiasi cha Tsh. billioni 2.5 zimeshatolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kisi kilichobaki kinatarajiwa kutolewa.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndugu Moses Nduligu mwenye shati jeupe akisaini kitabu cha mkataba
Awamu ya kwanza ya ujenzi itahusisha jengo la mbele ambapo kiasi cha Tsh. 4,767,886,814 zinatarajiwa kutumika.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ndugu Christino Mufoga akiongea wakandarasi waliokuja kusaini mkataba
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.