Mtaalamu wa Ufugaji Samaki Kutoka Kampuni ya Aquatel Fish Farming Consultancy Toka Mwanza Bw. Simon C. Akiwa na Furushi la Vifaranga wa Samaki Tayari Kwa Kupandikiza Majini.
Kushoto ni Dereva wa Halmashauri Bw. Budoya
Baada ya Kushushwa Kutoka Kwenye Gari Vifaranga Hao wa Samaki Sato Walipelekwa Hadi Sehemu ya Kupandikiza Bwawa la Dongobesh Kama inavyoonekana.
Aliyevaa Kofia Nyekundu Kushoto ni Afisa Mipango (W) Bw. F. Kundi na Kulia Aliyenyanyua Mikono ni Afisa Mifugo na Uvuvi (W), Bw. Moses Nduligu.
Mtaalamu wa Samaki Bw.Simon C. Saji wa Kampuni ya Aquatel Fish Farming Consultancy Akiwa na Kifaa Maalumu Yaani kipima joto "Thermometer" cha Kupima Joto la Maji Husika.
Upandikizaji Likiendelea Katika Bwawa la Dongobesh Mbulu.
Hapo Sio Kigamboni Dar es salaam ni Dongobesh - Mbulu, Muonekano wa Bwawa la Dongobesh.
Huo ni Mfereji wa Umwagiliaji Uliyotengenezwa Kisasa kwa Kuweza Kuyaruhusu Maji Kiasi Kinachotakiwa Kwenda Mashambani. Hao Unaowaona ni Ndege Walao Viumbe vya Majini Waitwao Kurastara, Wanapatikana Hapa Kama Unavyowaona Mpenzi Msomaji.
Mtambo wa Kusukuma Maji Kiasi cha Kilometa 4 Hadi Kufikia Mashamba Husika Ili Katika Kilimo cha Umwagiliaji Kata ya Dongobesh - Mbulu.
Upandikizaji Likiendelea Katika Bwawa la Mangisa.
Muonekano wa Bwawa la Mangisa.
~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~
Katika kuhakikisha Halmashauri inaongeza mapato ya ndani ili kuweza kuongeza nguvu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kupitia idara ya mifugo na uvuvi watimiza azima ya kupanda vifaranga 15,000 vya samaki aina ya Sato katika mabwawa 3 yaani bwawa la Dongobesh, Mangisa na Muslur tarehe 16.10.2021. Katika kazi Hii kampuni ya Aquatel Fish Farming Consultancy toka Mwanza ndiyo iliyoshida tenda ya upandaji huu ambapo mtaalamu wa Samaki hawa bwana Simon C Saji wa kampuni hiyo alianza kwa kupima joto la maji ya bwawa husika na kifaa maalumu yaani kipima joto "Thermometer" kisha zoezi la kuwapanda ndipo liliendelea.
Kuhusiana na zoezi hili wataalamu hawa walifika miezi kadhaa nyuma kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu juu ya mabwawa haya kwa aina ya maji, joto la nje na ndani ya maji, aina ya vyakula vilivyopo , muelekeo wa maji ulivyo kikondo na uwingi wa maji ya bwawa husika ambapo katika utafiti huo ndiyo uliopelekea kufanya maamuzi ya kupandwa samaki hawa.
Taarifa za wataalamu hawa wamesema samaki hawa watakuwa hadi kufikia wakubwa kwa muda wa miezi 3 ambapo hapo na wao wataanza kujamiiana na kuanza kutaga mayai ambapo baada ya miezi 3 tena samaki watakuwa tayari ni wakubwa na kuanza kuvunwa kwa ajili ya matumizi ya chakula kwa binadamu. Hivyo wananchi wameaswa kutoshiriki katika zoezi lolote la kuvua hadi hapo watakapotangaziwa rasmi kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya hawa samaki kuzaliana kwa wingi.
Kimsingi samaki pia ni kitoweo tosha kwa wananchi kwa chakula kwa kuongeza protini mwilini inayojenga mwili na kulinda pia, na zoezi la uvuvi litakapokuwepo hapa itaibua biashara nyingi "associative business" kuanzia mama lishe, usafirishaji, vituo vya kuweka na kutoa fedha kwa njia ya mtandao na mengine mengi hivyo ajira kupatikana na kuongeza mzunguko wa kifedha katika maeneo haya na Wilaya kwa ujumla wake. Imefahamika kwamba katika mabwawa haya awali yalikuwa yanatumika katika kilimo cha umwagiliaji wa mimea kama vile vitungu maji, vitunguu swaumu, kariti na mazao mengine ya biashara kazi inayoendelea hadi sasa kwa kutumia mitambo ya kusukuma maji kwa umbali wa hadi kilometa 4.
Haya hayaji tu kutoka hewani bali ni mipango thabiti ya Idara ya husika ya Mifugo, Menejimenti ya wataalamu kwa ushirikiano wa Baraza la madiwani katika lengo kuu la kupata fedha zitakazotatua kero mbalimbali za wananchi.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.