Kama Inavyoonekana Katika Picha ya Hapo Juu, ni Afisa Mifugo Bw. Richard Akiendelea na Zoezi la Kuchoma Chanzo ya CBPP Katika Viwanja Vya Kituo cha Kuchanja Mifugo Mkabala na Stendi Kuu ya Mabasi ya Dongobesh.
Kama Inavyoonekana Katika Picha za Hapo Juu, Wananchi Wakiswaga Mifugo Yao Ndani ya Uzio wa Chanjo Tayari Kwa Chanjo Katika Viwanja Vya Kituo cha Kuchanja Mifugo Mkabala na Stendi Kuu ya Mabasi ya Dongobesh.
Katika Picha za Hapo Juu, Kutoka Kushoto ni Afisa Mifugo Kata ya Dongobesh Bi. Flora Semitende Akitoa Risiti ya Kielektroniki Kwa Kutumia "POS" Baada ya Kumhudumia Mwananchi Petro Naaman Aliyechanja Mifugo Yake.
Baadhi ya Mifugo Ikisubiri Kuingia Kwenye Uzio Huo Ili Kupata Chanjo Katika Viwanja hivi.
Baadhi ya Mifugo Ikiondoka Kituoni Hapo Baada ya Kupata Huduma ya Chanjo Hiyo.
Baadhi ya Wataalamu wa Mifumo Ikiwa ni Kikosi Kazi cha Zoezi la Chanjo Wilayani Mbulu.
Afisa Mifugo wa Kata ya Tumati Wilayani Mbulu kiwa Miongoni mwa Kikosi Kazi Hiki Katika Kutoa Huduma Hii Muhimu kwa Wananchi.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Katika kuhakikisha wananchi wananufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo mifugo kama vile ng'ombe, wananchi hawa wameamua kujitokeza kwa wingi katika uchanjaji wa mifugo yao ili waweze kupata faida kupitia mifugo yao baada ya kuwa na uhakika wa kuishi kutokana na kupata chanjo ya homa ya mapafu (CBPP) ambayo ni kinga ya ugojwa huu unaosumbua sana mifugo hii kwa rika zote.
Haya yamejiri leo katika zoezi endelevu la uchanjaji mifugo zoezi lililofanyika jana na leo kijiji cha Dongobesh kata ya Dongobesh ambapo ng'ombe takribani 1538 wamechanjwa leo katika kituo cha kuchanjia mifugo mkabala na stendi kuu ya Dongobesh. Ratiba ya kuendelea vijiji vingine itapangwa kijiji gaji na kata ipi ya kuendelea nayo ambapo hufanyika siku 2 kwa kila kijiji cha zoezi la uchanjaji huu. Hata hivyo kabla ya kutoa huduma hii hapa, kikosi kazi hiki kilikuwa kata jirani ya Tumati ambako mifugo ipatayo 2475 ilichanjwa.
Tunaishukuru Serikali kwa kuwaajiri hawa wataalamu wa mifugo kupitia Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambapo huduma hii inatolewa kwa wananchi kwa bei elekezi ya Tshs. 500/= kwa ng'ombe mmoja ambapo risiti ya kielektroniki hutolewa kwa mteja kama kithibitisho na kuhakikisha fedha hizi zinakuwa salama ili tuweze kununua madawa ya chanjo nyingi nyingi zaidi.
Kwa msisitizo, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji bado inawahimiza wananchi kuitikia mwito huu zaidi hususani kwa maeneo yanayo endelea kuchanja ili kuwa na uhakika wa faida ya mifugo kwa kutoathirika na homa hii mbaya kwa mifugo yao.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.