Akiongea na Wakuu wa Shue za Msingi,Sekondari na Maafisa Elimu Kata wapatao mia mbili thelathini na sita ( 236) katika Viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Komredi Heri James Mkuu wa Wilaya ya Mbulu amesema kuwa kutokana na kazi nzuri zinazofanywa na Walimu ameamua kuwaita kukaa na kupongezana pamoja,
Amesema Walimu ni chombo kilichobeba dhamana kubwa katika jamii, kwani wamekuwa na mchango mkubwa katika kulinda na kutunza Taifa hili. Wilaya ya Mbulu imebalikiwa kuwa na Walimu bora na mahiri kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hii, aidha kutokana na uwepo wao wamekuwa viongozi wazuri katika kutimiza na kutambua malengo yaliyo mbele yao.
Ameendelea kutambua mafanikio na michango katika maeneo yao mbalimbali ya kazi kwa kutambua utendaji wao wa kazi kwa kupitia matokeo mbalimbali ya mitihani.Pamoja na kuwa na viwango mbalimbali vya matokeo ameendelea kutaka kujua kama walimu hao wanaridhika na kile wanachokifanya, ili kuonesha kuwa wamekuwa hawaridhiki na kile wanachokifanya ndio maana walimu hawa wamekuwa wakipambana kila kunapokucha kuweza kuendelea kuboresha zaidi matokeo kwa viwango tofauti tofauti vya juu.
Amesema kumekuwa na jitihada mbalimbali za kuwaboresha walimu masilahi yao ya Utendaji ambapo amewaagiza Maafisa watumishi kuendelea kurekebisha madai mbalimbali ya walimu kama vile Uhamisho, madaraja na malimbikizoya mishahara kwani Serikali imekuwa na jitihada za dhati katika kuimarisha, kuboresha na kujenga miundo mbinu mbalimbali kwa kupitia miradi tofautii tofauti.
Amewaomba walimu kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kutunza heshima yao waliyonayo katika maeneo mbalimbali na sio kuwa chombo cha adhabu kila eneo kwani jamii imekuwa na imani sana nasi, niwaombe Maafisa elimu kata kuwa ni chachu ya kusimami kwa dhati elimu katika maeneo yao ya kazi na kuhakikisha wanaweka ratiba nzuri ya ufatiliaji wa maendeleo ya elimu katika kata zao ili waweze kuwapunguzia maafisa elimu kazi ya kuita walimu ofisini.
Anapenda kuwapongeza Wakuu wa shule kwa kusimamia vizuri Walimu ,Wananfunzi, na Wazazi na walezi walionao katika Jamiii, ni ndoto yetu kuona makundi hayo aliyoyataja yanasimamiwa kwa ufasaha kwani yanapotoka mafanikio yanaanza kwa kutajwa mwalimu Mkuu aliyekuwa daraja la mafanikio hayo ili kuyafanya hayo lazima tuimarishe mahusiano baina yetu katika taasisi zetu kwani msingi wa mahusiano ni mawasiliano
“Amewataka walimu kuungana kwa dhati juhudi za kuboresha maadili na kukemea mmonyoko mkubwa unaolikumba Taifa kwa sasa, amewaomba kusimama kwa pamoja kulinda Taifa letu lililo katika vita mbaya ya kupambana na kupinga vitendo vya ubakaji, usagaji, ufisadi, ulawiti ili kuwandaa watoto wetu kwa kizazi kijacho”.
Katika kupambana na hayo yote yanasiamaiwa na mambo matano katika wilaya yetu,ambayo ni kusimamia kwadhati Utawala wa Sheria,Haki, Usawa,Maendeleo,Umoja na Haki. Ili Kuendeleza juhudi za kupandisha ufaulu amewasisitiza Walimu kuzingatia yafuatayo:-
Kusimamia maadili ya watoto na watumishi katika maeneo yetu
Kuheshimu misingi ya taaluma, maadiliya kazi na kuheshimu utaratibu wa utumishi wa Umma
Kuheshimu taratibu za kazi walizojiwekea
Wakiongea kwa nyakati mbalimbali Wakurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya na Mji wamepongeza kwa tukio kubwa la kuwaita Walimu Wakuu wote wa shule za Sekondari na Msingi kwa utendaji wao wa kazi, Wamewaomba Walimu kuendelea mshikamano wao wa pamoja katika kazi za kujenga na kuimarisha taaluma. Kitabu cha “The Power of Teachers” aliandika Mwalimu Nyerere kwa mwaka 1969 kikieleza kwa jinsi walimu wakitaka kuliangusha Taifa wanaweza na wakitaka kulijenga Taifa, kwani wao ndio wamekuwa na jukumu kubwa la kutunza, kulinda na kujenga maadili ya watoto na pia wamekuwa wasimamizi wazuri wa miradi ya maendeleo katika shule zao wanayopelekewa na Serikali. Tuanawaomba walimu waendelee kuwa chachu ya kusimamia,kudumisha na kulinda maadili ya watoto licha ya kuwa na vikwazo mbalimbali na tusisite kutoa taaraifa yoyote ya uvunjifu wa maadili katika jamii inayotuzunguka.
Niombe makundi ya vyama vyenu yasiwe chanzo chakushusa Elimu au mmonyoko wa maadiliya Walimu,ni vyema tukae tuondoe tofauti zetu kupitia wawakilishi wa vyama hivyo, “amehitimisha kwa kusema hayo Komredi James”
“KWA PAMOJA TUNAIJENGA MBULU YETU”
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.