Magreth Mbawala, Mbulu DC,
Katibu wa afya wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu bwana Pascas Isondo ambaye amemwakilisha mganga mkuu wa wilaya amewataka wamiliki wa vituo vya Watoto wasajili vituo vyao kwenye mamlaka husika na vitambulike ili waweze kutoa huduma.
Baadhi ya walimu wakiwa wanafuatilia masomo katika semina iliyokuwa inaendelea.
Hayo yalisemwa na katibu wa afya wa wilaya bwana Pascas Isondo wakati wa kufunga mafunzo ya walimu na taasisi zote zinazohusika na malezi ya Watoto chini ya umri wa miaka mitano,yaliyofanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 11-15 Novemba 2024 na kuhudhuriwa na walimu 35, katika ukumbi wa kanisa la TAG Dongobesh.
Walimu na wakufuzi wakiwa kwenye picha ya pamoja, baada ya kumaliza mafunzo.
“Ninyi ni mfano mzuri sana wa kuigwa kwa malezi na makuzi ya Watoto wetu hivyo mkazingatie vizuri elimu mliyopewa hapa na myafanyie kazi ili tuweze kuwa na vituo ambavyo Watoto wetu watapata malezi yanayotakiwa.” alisema Isondo.
Naye mkufunzi wa mafunzo bwana Chriss Madaha kutoka Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum alisema mafunzo haya yanawalenga wamiliki wa shule za Watoto wadogo (daycare) na taasisi nyingine kama nyumba za Watoto yatima na nyumba salama,ikiwa na shabaha ya kuunga mkono serikali kuboresha malezi kwa kuwa na watoa huduma wenye elimu ya malezi.
Pia bwana Madaha alisema hii ni awamu ya pili kufanya mafunzo haya katika halmashauri ya wilaya ya Mbulu na yatakua endelevu kutokana na uhitaji wa jamii husika.
Aidha mkuu wa kitengo cha ustawi wa jamii Ezekiel Assecheck aliwashukuru taasisi ya Birth Hope Centre kwa ufadhili wa asilimia mia kwa watu thelathini na kuweza kufanikisha mafunzo hayo pia alitoa wito kwa walimu na walezi wasiokua na mafunzo wajitokeze ili kupata elimu kwa wakati mwingine.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.